Wednesday, March 8, 2017

Vita vya Panzi

Vita vya panzi Furaha ya kunguru
Wao wanakufa wawala kunguru
Hata kama hawajui wale wala kuru
Panzi wakikukuruka furaha yao Kunguru

Furaha yao kunguru panzi wakikukuruka
Hata wakitaka kwenda wao wataruka!
Lakini kunguru aweza kuruka kushinda panzi
Panzi wakikukuruka furaha yao Kunguru

Panzi yeye mnyonge kwani huliwa haraka
Kunguru analo domo laweza daka haraka
Wawili panzi au watatu kunguru aweza kudaka
 Panzi wakikukuruka furaha yao Kunguru

Japo umoja ninguvu si kwa hawa nyangarika
Hata wawe maelfu bado watanyanyasika
Kunguru akisha tua panzi wanaweweseka
 Panzi wakikukuruka furaha yao Kunguru

Mwisho mimi namaliza Kaditama nimefika
Babu labda atanipa jibu ninalolitaka
Kuhusu huu umoja ambao hamna muafaka
Panzi wakikukuruka furaha yao Kunguru