Wednesday, March 30, 2016

Jinsi Ya Kuandika Barua ya Kuomba Mkopo Benki

“People who ask confidently get more than those who are hesitant and uncertain. When you've figured out what you want to ask for, do it with certainty, boldness and confidence. Don't be shy or feel intimidated by the experience. You may face some unexpected criticism, but be prepared for it with confidence.” ― Jack Canfield Ndugu wasomaji wa makala zangu. Habari za leo. Naomba leo nitoe changamoto ya Jinsi ya Kuandika barua ya maombi ya mkopo. Hii naita changamoto kwani kuna njia mbali mbali za kuandika barua za namna hii. Baadhi ya vyombo vya fedha hutoa fomu ambayo inakuongoza hatua kwa hatua mambo ya kujaza na ukisha jaza basi unakua umesha eleza mambo yote yanayotakiwa. Lengo la mada hii ni kuchokoza fikra za ubunifu wa “wewe” au “sisi” wenyewe kuwa ndio chanzo cha kuanzisha wazo la kuomba mikopo kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya fedha vilivyopo katiak maeneo yetu. Nitapenda sana kama nitasikia kutoka kwenu kama kuna mtu ambaye ameweza kuandika barua yake ya kuomba mkopo na mkopo ukakubaliwa. Kama taniruhusu nitaiweka wazi kulingana na matakwa yake. Nikiwa na maana kama atataka tutumie majina yake halisi ama la, basi tutafanya hivyo hivyo kulingana na matakwa yake lengo ni kujifunza. Basi leo sitaki kuchukua mud asana nakala ya barua iko hapo ukurasa unaofuata. Mika Ayo- Mwalimu Asanteni MIRISHO MASAI ALEI S.L.P 7443, ARUSHA 23/09/2015 MENEJA MKUU, BENKI YA WANANCHI WETU, S.L.P 20,000 USA RIVER, ARUSHA YAH: MAOMBI YA MKOPO WA TZS 3,410,800 KWA AJILI YA KUENDELEZA MRADI WA UFUGAJI WA SUNGURA. Husika na somo la hapo juu, Mimi ni mkazi wa mjini Arusha Kata ya Muriet. Kwa jina ni Mirisho Masai Alei kama ilivyo kwenye anuani hapo juu. Mimi ni Mteja wa Benki yenu mwenye akaunti namba 002 inayojulikana kwa jina la Mirisho Masai Alei ambayo ndiyo nitakayoitumia kupokelea mkopo na baadaye kulipia mkopo wangu pindi utakapo kubalika na kupitishwa. Kusudi la barua hii ni kuomba mkopo wa shilingi 3,410,800/ (milioni tatu na laki nne na elfu kumi na mianane tu) kwa ajili ya kukuza mradi wangu wa ufugaji wa sungura. Mradi kwa sasa umeshaanza na wana idadi ya sungura wapatao 14. Kati ya hao majike ni 10 na dume ni 4. Sungura hao majike 10 watatumika katika kuzalisha watoto kwa ajili ya kuuza sokoni kama ilivyoelezwa kwenye barua hii hapochini. Mradi wote utagharimu kiasi cha shilingi 4,643,800/ (milioni nne laki sita arobaini na tatu elfu na mia nane tu). Kiasi kinachoombwa benki ni sawa na asilimia 73.45 ya mradi wote na muombaji atatoa asilimia 26.55 ya gharama yote ya mradi. Dhamana ya mkopo ni kiwanja changu kilichoko kwenye eneo la Lolovono chenye ukubwa wa mita 14 x 22 chenye thamani ya shilingi 6,000,000/ (milioni sita) katika eneo ambalo halijapimwa. Nakala ya hati pamoja na barua ya mtendaji wa Kata vimeambatanishwa na barua hii kuthibitisha uhalali wa umiliki. Matarajio kutokana na utaalam wa ufugaji wa sungura ni kwamba uzalishaji utaanza baada ya miezi sita tangu mradi kuanza. Aidha mradi unatarajiwa kuzalisha faida ya shilingi 400,000 kwa mwezi, kama Benki itakubali kuanza kupokea malipo ya mkopo huu kidogo kidogo, kwa maneno mengine fedha yote ya faida ni wazi kwamba mkopo huu utakuwa tayari umeshalipwa baada ya mwaka mmoja baada ya mradi kuanza uzalishaji. Hii ni sawa na kusema kuwa mkopo utaisha kulipwa baada ya miezi 18 tangu ulipotolewa. Soko la sungura nina mkataba wa kisheria na Kampuni ya Positive Eye kwa miaka sita wa kisheria wa kuwauzia sungura. Nakala ya mkataba wa uhakika wa kuuza sungura umeambatanishwa hapa. Ni matumaini yangu kuwa ombi langu litakubaliwa , Asante. Mirisho Masai Alei.

Sunday, March 27, 2016

JINSI YA KUPATA UHURU WA KIPESA

Ndugu wasomaji wa makala zangu. Leo naona tuzungumzie uhuru wa kipesa (Financial freedom). Jambo la kwanza kabisa,tujiulize; Uhuru wa kipesa ni nini? Ni hali ya kuwa na kipato cha uhakika kinachokutosheleza kuendesha maisha yako kwa kiwango ulichojipangia bila kutetereka kwa maisha yako yote bila kuhitajika wewe mwenyewe kufanya kazi. Hapa pesa inakuwa ndiyo inayo kutumikia. Sio wewe kuitumikia fedha! Kabla sijagundua siri hii nilikuwa kama watu wengi walivyo na wanavyoendesha maisha yao. Anaanzisha biashara ili apate pesa zaidi. Anaenda kuongeza elimu ili apate kazi nzuri zaidi. Ataandika barua ya kuoomba kupandishwa daraja ili apate fedha zaidi. Atabadilisha kazi ili apate pesa zaidi. Orordha hii ni ndefu sana. Lakini nikaja kugundua kuwa kumbe siri sio kupata pesa nyingi zaidi bali siri ni hii. Ni kiasi gani kinakubakia mkononi baaday ya kulipwa pesa yako kama ujira au mauzo ya bidhaa au biashara yako? Mfano kama unapokea mshahara wa shilingi 500,000 kwa mwezi na unamatumii yafuatayo: Kodi ya nyumba shilingi 50,000 hii inamaana ndani ya ile hela ulionayo 50,000 ni ya mwenyenyumba wako. Kama una bili ya shilingi 120,000 dukani ambayo utatakiwa kulipa basi hiyo shilingi 120,000 si ya kwako ni ya mwenye duka. Kama unatakiwa kulipa ada ya shilingi 200,000 basi hiyo hela si yako ni ya shule au chuo anako soma mwanao. Unaweza kuona katika shilingi 500,000 umebaki na shilingi 130,000 na hapo bado mahitaji mengine kama vile umeme, maji, nauli ya kwenda na kurudi kazini. Hivyo ukiangalia utaona kuwa unaweza kubaki huna kitu baada ya kutoa matumizi yote. Lakini ziko mbinu za kufanya au njia ya kufuata ili ubaki na kitu. Ila tujiulize swali moja kwanza, je, pesa zaidi yaweza kutatua tatizo la kipesa? Watu wengi ukiwauliza swali hili bila kusita watakuambia ndiyo! Lakini wataalam wamegundua kuwa pesa zaidi badala ya kutatua tatizo la pesa huongeza matatizo ya kipesa makubwa zaidi! Ukiangalia kwa kina watu wengi wenye kipato kikubwa kwa maana ya mishahara mikubwa au kipato kikubwa ukiwachunguza wengi wanapokea fedha hizo kwa mkono mmoja na kuzitoa zote kwa muda mfupi kwa mkono wa pili. Kwa njia gani? Kulipia mikopo ya magari, nyumba na kadhalika. Shida kubwa hapa inakuwa siyo mkopo au kukopa shida ni kuwa mikopo mingi inakuwa inatuweka kwenye utumwa wa madeni ambao unatuweka kuwa na shida ya pesa zaidi au masikini wa kutupwa siku zetu za uzeeni. Na ukumbuke tunahitaji kujikomboa kabla hatujashindwa kufanya kazi hivyo nakushauri uchukue hatua. Ili kujikomboa kifedha jaribu kufuata kanuni ifuatazo. 1) Weka mpango wa lini unataka kustaafu (kustaafu siyo tu kwa waajiriwa hii ni kwa kila mtu, kumbuka kuna umri utafika huwezi kufanya tena kazi kutokana na kuwa mzee) Katika hatua hii unajiwekea umri ambao unaweza kustaafu. Kwa hapa Tanzania umri wa serikali wa kustaafu kwa hiari ni miaka 55 na kustaafu kwa lazima ni miaka 60. Sasa kwa kufuata umri huu wa serikali basi unaweza kuweka malengo yako ya muda wa kustaafu kuwa umri huo au hata unaweza kujiwekea umri wa chini kidogo au wa juu kidogo. Pia weka kiwango cha pesa ambacho vitega uchumi vyako vitakuingizia. Kiasi kiendane na mambo makuu matatu. Moja Mtindo wako wa maisha unaotaka kuishi baada ya kustaafu (kumbuka aina ya maisha utakayochagua kuishi baada ya kustaafu ndiyo itakuongoza kuweka kiwango chako cha pesa itakayoingia kwa mwezi toka kwenye vitega uchumi vyako), Jambo la pili ni kuzingatia kushuka kwa thamani ya pesa, kumbuka pesa inashuka thamani kila siku (hili ni tatizo la sarafu zote hapa duniani tofauti ni kwamba kunazinazoshuka kwa kasi zaidi na nyingine hushuka taratibu kulingana na nguvu ya uchumi wan chi husika lakini sarafu zote hushuka thamani). Jambo la tatu ni uhakika wa vitega uchumi vyako kuendelea kuzalisha hela hata kama hali ya uchumi wa nchi au dunia itabadilika. Hii ni muhimu sana kwani miaka ya 2007/8 wakati wa mtikisiko wa wa uchumi wa dunia watu wengi walio kuwa wamewekeza kwenye masoko ya hisa walipata hasara kubwa sana. Sisemi kuwa masoko ya hisa ni mahali pabaya pa kuwekeza ila inatakiwa ujifunze jinsi ya kuwekeza ili uweze kupata faida wakati wote. Kwani masoko ya hisa ni moja ya sehemu ambayo unaweka pesa na pesa yako inakufanyia kazi. Wewe umelala bado pesa inaingia lakini inahitaji kuwa na elimu kwenye mambo hayo na hii ni moja ya malengo ya mimi kuanzisha blog hii ili tuweze kupeana mawili matatu juu ya kujikwamua kiuchumi. 2) Weka akiba Watu wengi ukizungumzia habari ya kuweka AKIBA watakuambia kuwa hawana pesa ya kuweka akiba! Ukweli ni kwamba kuweka akiba ni suala la tabia na sio kuwa na fedha nyingi ama kidogo. Ukumbuke kuwa akiba hii hutaitumia kabisa, ila badala yake utaiwekeza ili izidi kukuzalishia pesa zaidi. Tabia ya kuweka akiba ni tabia ya kudumu sio suala la muda fulani tu, tabia hii huwa ni ngumu sana kujenga. Hii inatokana na kuwa hatujajengewa tabia ya kuweka akiba tangu tukiwa wadogo. Shuleni hakuna somo la kuweka akiba, chuoni hakuna somo la kuweka akiba. Ila tukianza maisha ndipo tunakutana na vitu kama Vyama vya Akiba na Mikopo. Wakati akili zetu zimesomeshwa Mikopo na Akiba, ndiyo umesoma sahihi Mikopo na Akiba. Au ili unielewe kirahisi Matumizi na Mapato. Watu wengi wanaishi kwa kukopa kopa kutokana na malezi tulio kulia. Ukitaka kitu baba au mama anakupa pesa ya kununua. Ulipokuwa chuo kwa wale waliobahatika kwenda vuo hasa vile vya Elimu ya Juu, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inakupa mkopo. Na tukisha pewa hizo fedha tunazitumia bila kufikiria kesho kwa nini? Baba au mama au kuna mtu mwingine anawajibika kutupa pesa ili tuzitumie kutatua matatizo yetu! Hakuna mtu anafikiri KESHO yaani kuweka ‘AKIBA’ . Nisisitize tu kuwa kuweka akiba sio suala la kuwa na fedha nyingi ni suala la kujenga tabia. Ujue ukiweza kujenga tabia hii ujue kuwa uko njiani kufikia kwenye UHURU wa KIPESA . 3) Punguza matumizi yasiyo ya lazima Kwa kawaida kuna matumizi ya lazima na matumizi yasiyo ya lazima. Kwa mfano – Kwenda disko wakati unaishi nyumba ya kupanga sio sahihi. Kununua nguo ambazo kwa kweli si lazima pia haina sababu. Mimi sitaki kuingilia uhuru wa mtu lakini hebu fikiria ni kipi ungechagua kama ungeambiwa kuwa vumilia wiki moja bila kuoga, ili Yule anaye kuletea maji ya kuoga kutoka mbali (pesa) aende akashiriki kuchimba mtaro na kutandika bomba halafu baada ya wiki utapata maji ya kuoga muda wote na kila mara maji ambayo yatakuwa ya uhakika na yakutosha kwa maisha yako yote au uwe unapata maji ya kuoga kila siku lita tatu tu tena kwa shida! Wengi kwa haraka tungesema tuko tayari kuteseka wiki moja halafu tupate uhuru wa maji. Lakini ukikaa siku tatu bila kuoga, unanuka! hujafua nguo pengine unaanza kupata chawa unajikuta unaanza kushawishika kupokea lita 3 ili angalau upata raha japo si ya muda mrefu wala si kamili. Mara nyingi kwenye suala la pesa ndivyo tunavyochagua raha ya muda mfupi tunaacha ile raha ya kudumu japo inagharama kidogo! Tunachagua raha ya muda mfupi sana halafu tunateseka maisha yetu yote! Kama unataka kutoka kimaisha amua kwa dhati kuchukua hatua. PUNGUZA MATUMIZI YASIO YA LAZIMA WEKA VIPAUMBELE USIFUATE MKOMBO. Nikuambie tu kwamba wewe unabahati sana una mahali unasoma, hata kuna watu wameandika vitabu juu ya mada hii. Jambo ambalo kwa siku hizi elimu hii hutolewa redioni, kwenye TV kwenye blog na maeneo mbalimbali. Swali ni je, ni nani atachukua hatua kuyatendea kazi? Kumbuka waswahili husema “HAJA YA MJA HUNENA, MUUNGWANA NI VITENDO” kumbuka mambo haya kama utaamua kuyafanyia kazi maisha yako yataanza kubadilika. 4) Anza kujifunza kuwekeza pesa yako Watu wengi hasa waajiriwa tegemeo lao kubwa ni akiba wanazowekewa kwenye mifuko ya jamii na mwaajiri (social security funds)na ni kawaida siku hizi kusikia mtu fulani amestaafu na amelipwa mamilioni ya pesa. Na wengi wakisikia hivyo wanahamasika kuendelea kufanyakazi ili baadaye walipwe mamilioni ya pesa. Sina shida na mtu aliye chagua maisha kama hayo ya kuajiriwa maisha yote, ila tu shida yangu ni hii moja. Je, wewe ulikuwa na mshahara wa shilingi milioni 4 kwa mwezi wakati unastaafu. Leo unalipwa milioni 80 kwa mkupuo na akili yako ndo ile ya matumizi na mapato badala ya mapato na matumizi hivi hiyo hela unakaa nayo kwa muda gani kabla haijakatika? Mimi ninaye andika hapa nilikuwa mfanyakazi wa serikali miaka ya mwishoni mwa 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90 nilikuwa kijana wakati ule na serikali ikaanza zoezi la kupunguza wafanyakazi. Watu walikuwa wakipunguzwa na ukisikia wakati ule mtu amelipwa shilingi 300,000 mwili unasisimka kwani kwa thamani ya pesa ya wakati ule ilikuwa nyingi sana! Lakini cha kushangaza karibu wote wale angalau niliowafahamu wengi walifilisika, baadhi yao walikufa kwa kihoro, na wengine wachache waliomba kazi kwenye taasisi nyingine na ninaye mkumbuka mmoja tu, ndiye aliye weza kutoka kimaisha! Ninacho kuambia ni kwamba usikubali hatima ya maisha yako iwe mkononi mwa mtu mwingine. Wewe unawajibika na maisha yako! (Mimi niliamua kuondokana na mfumo huo na kufuata mfumo mwingine lakini hiyo ni hadithi ya siku nyingine)! Leo hii zaid ya wa-Tanzania 90% wakiwemo wasomi wa vyuo vikuu hawajui ni nini maana ya hisa, hati mfungani na hata mifuko kama ya UMOJA FUND. Hawajuhi ni namna gani wanaweza kutumia fursa zilizopo hapa nchini ili kuweza kujikwamua kimaisha! Laiti tungejifunza kuwekeza fedha zetu hali yetu ya maisha ingebadilika! Ninajua baadhi ya watakao soma makala hii wanabiashara au miradi inayowaingizia pesa ya uhakika hivyo watasema ah; kwani kunashida gani nina kazi inayo niingizia mshahara mzuri na biashara zangu zinafanya vizuri. Vema, lakini nikuulize je, biashara hizo ni endelevu? Namaanisha una uhakika kuwa zitakupa kipato hivyo hivyo au kutakuwa na mabadiliko? Jibu unalo kutokana na wale waliofanya biashara kama unayofanya na kwa mfumo unao tumia wewe. Kama mfumo unaotumia ni sahihi basi hongera kama siyo sahihi basi anza kufikiri juu ya namna bora au mfumo bora wa kukupatia kipato. Kumbuka kazi yako hutamwachia urithi mwanao ila kama una hisa, au kampuni inayofanya vizuri iliyoanzishwa kitaalamu basi utaweza kumwachia mwanao urithi. Jifunze na namaanisha kwa kuingia shule ya vitendo, jifunze kuwekeza fedha zako kwa faida zaidi na kwa njia endelevu. 5) SOMA ELIMU YA UWEKEZAJI Jambo jingine muhimu kama unataka kujikwamua kifedha ni kusoma elimu ya uwekezaji. Kuna watu wengi sana wameandika vitabu vyao vya Kingereza na vya Kiswahili na hapa nitakutajia vitabu vichache lakini muhimu ni wewe kufanya jitihada za kujisomea hasa ukilenga kujua zaidi juu ya uwekezaji unaotaka kuutumia katika kukuingizia kipato. i) HISA, AKIBA, NA UWEKEZAJI ni Kitabu kizuri sana hasa kwa wale wanao taka kuwekeza kwenye Hisa, Akiba na hati fungani kinapatikana maduka yote ya vitabu Tanzania. Kimeandikwa na Emilian Busara na Mrembo Grace ii) Jinsi ya Kuwa Tajiri ni kitabu kizuri kwa mtu anayetaka kujifunza nidhamu ya kutumia pesa kwenye biashara na maisha ya kawaida. Kitabu kimeandikwa na Joseph Mayagila hiki kinapatika pia kwenye maduka ya vitabu. iii) Rich Dad Poor Dad Kitabu kimeandikwa na Robert T. Kiyosaki Kimeandikwa kwa lugha ya kingereza pia anazo nakala nyingi sana za Rich Dads ambazo zinpatikana madukani. Ukisoma vitabu hivi hutakuwa kama ulivyo. iv) Secrets of the Millionaire Mind. Ni kitabu kizuri sana kwa mtu anayetaka kubadili jinsi anavyofikiri kuhusu pesa v) 26 secrets How to defeat Your Enemies and Make Millions of Dollars- Kimeandikwa na Eric Shigongo James- hiki ni kitabu kizuri kwa wewe ambaye unataka kujua jinsi ya kupenya masoko mapya na jinsi ya kuingia mikataba na watu mbalimbali tofauti. Naona leo niishie hapa naamini kuwa utachukua hatua nilizo kushauri hutakuwa kama ulivyo. Wewe ni wa tofauti sana na unacho kitu cha ziada ndiyo maana umeweza kusoma makala hii yote. UTATOKA KIMAISHA! HONGERA! Nakutakia kila la heri. Mika Ayo - Mwalimu

Thursday, March 24, 2016

JINSI YA KUONGOZA WATU

Wapenzi wasomaji wa makala zangu, Karibuni tena tushirikishaneili kujifunza, jinsi ya kuongoza watu. Miongoni mwa jambo kubwa sana katika miradi, biashara, siasa, madhehebu ya dini na kadhalika ni “UONGOZI”. Ukiona katika biashara ofisi au hata mahali popote mambo yanaenda vizuri au hayaendi vizuri basi ujue uongozi unahusika kwa sehemu kubwa katika mafanikio au matatizo unayoyaona mahali husika. Kuna tofauti ya “kiongozi” na “meneja” ili kuweka mambo haya vizuri naomba nieleze tofauti iliyoko kati ya Meneja na “Kiongozi” “Meneja” Huyu yeye husimamia watu na rasilimali zilizoko ili kufikia lengo lililo wekwa na shirika au kampuni. Hana maono hutumia taratibu, kanuni na sheria zilizopo katika kukamilisha au kufikia lengo, meneja sio lazima awe kiongozi ili afanikiwe ‘hapana’ . “Kiongozi” Huyu anazo sifa kuu tatu ambazo kwa kweli ndiyo wajibu wake kimsingi. Sifa ya kwanza ni: Kubeba maono kwa kingereza wanaita – Vision. Sifa ya kiongozi ni kuona au kuonyesha njia wapi wanapo kwenda. Mfano mzuri wa kiongozi ni Musa kwenye Biblia. Anawaambia wana wa Israel “Kwa kuwa BWANA Mungu wako, yu akuingiza katika nchi nzuri, nchi yenye vijito vya maji, na chemichemi, na visima vibubujikavyo katika mabonde na milima…..” Kitabu cha Kumbukumbu la torati sura ya 8:7-10. Musa anamaono ya kule anakowapeleka watu! Kiongozi huwa ana maono. Sifa ya pili ya kiongozi ni: Kuhamasisha “Inspiration” wakati fulani watu hukata tamaa kutokana na mambo kuwa magumu. Kipindi mambo yanapokuwa magumu hapo ndipo unaweza kujua kama wewe ni kiongozi ama la! Katika mahali ambapo uongozi unafundishwa kwa uhakika ni jeshini. Jeshini huwa kunakuwa na maono ambayo hubeba yule mkuu wa kikosi, halafu yale maono huvunjwa vunjwa kuwa majukumu ya kila siku madogo, madogo ambapo kazi moja wapo ya kiongozi ni kuhamasiha. Hapa ipo mifano mingi sana lakini nitakupa mitatu tu. a) Wakati Tanzania inaingia vitani dhidi ya Idd Amin wa Uganda hamasa ilikuwa “Apigwe nduli Amini” askari waliokwenda vitani wakikusimulia jinsi ambavyo kauli mbiu hiyo ilivyowapa motisha utashangaa. Askari walilala kwenye madimbwi ya maji usiku kucha na kushinda mchana kutwa, walitembea hadi nguo zikachakaa mwilini na viatu kuchakaa, lakini hawakukata tamaa hadi walipotekeleza kile walichoamini. Kuona Uganda yenye demokrasia ya kweli. b) Mfano wa pili wahamasa ni “Harambee” Nadhani umewahi kusikia msemo maarufu sana ulioanzishwa na wenzetu huko Kenya wakati wa harakati za kupigania uhuru wao. Mzee Jomo Kenyatta ali kuja na hamasa ya “Harambee”. Na kupitia kauli hiyo ya harambee wananchi wa Kenya waliweka nguvu pamoja wakajikomboa na sasa ni Taifa huru. Hadi leo huko Kenya wanatumia kauli mbiu hii ili kutatua matatizo ya jamii kwa pamoja! c) Kauli nyingine ni ile ya Maji Maji. Ingawa vita vya Maji maji vinaweza kuonekana kama havikufanikiwa lakini kwa kiasi kikubwa Mzee Kinjikitile Ngwale alifanikiwa sana kuwahamasisha watu kupigania haki zao kwa kuwaaminisha kuwa kwa kujipaka dawa maalum alioitoa risasi zitageuka maji. Watu waliamini na wakaingia vitani na wakaamini kuwa yeyote aliyepatwa na risasi ya mkoloni ni kwa sababu ya kutokuamini dawa aliyopewa ndipo madhara yakampata! Unaweza kuona nguvu yamotisha katika uongozi au hasa niseme toka kwa kiongozi. Kiongozi ni mtu mwenye uwezo wa kuwashawishi watu kufanya jambo analo taka lifanyike hata bila yeye wakati mwingine kulifanya. Sifa nyingine ya Tatu ya kiongozi ni : Kutoa motisha. “Motivation” Kiongozi anaye jua uongozi ni lazima hutoa motisha. Sasa hapa ifahamike kuwa kuna aina mbili za motisha. 1. Motisha Chanya Motisha chanya hii hutolewa kwa kumpongeza mtu kwa kufanikisha kazi katika eneo analosimamia. Huwa inatolewa kwa maneno ya pongezi, kupewa zawadi fulani na hata wakati mwingine kupandishwa daraja au kupewa cheo cha juu. 2. Motisha Hasi Motishahasi halikadhalika hutolewa kwa njia ya maneno kama karipio kali, kushushwa cheo na hata kwa baadhi ya viongozi hufikia hatua ya kuua mtu aliyeshindwa kufikia malengo yake kwa uzembe! Uongozi (leadership) ni kipaji ambacho watu wachache uzaliwa nacho. Lakini ni kipaji ambacho kila mtu anatakiwa kuwa nacho bila kujali kazi anayofanya, ngazi yake ya uongozi au cheo alichonacho. Kwa kuwa kuna watu wachache waliozaliwa wakiwa viongozi basi sisi wengine inatupasa kujifunza. Tunajifunza kwa kusoma makala kama hii unayosoma, kusoma vitabu vya viongozi wakubwa kama akina Martin Luther King, Nelson Mandela, Barak Obama na wengine. Kikubwa unachotakiwa kufanya unapoongoza watu ni kuhakikisha kuwa unakuwa kwenye huu mstari wenye mihimili mitatu. Maono (Vision) Hakikisha kila mtu kwenye shirika ofisi au kampuni anafahamu maono au ndoto ya kampuni yenu. Hakikisha kila siku wewe na timu yako mnachokifanya kina lengo la kutimiza maono yenu au ndoto ya Kampuni Hamasa (Inspire) – hakikisha wewe kama kiongozi unawapa watu hamasa. Hata kama kwa sasa uko peke yako unayetekeleza maono yako fuata kanuni hizi, Jipe hamasa ya kufanya kazi kwa kujitia moyo jiambie “NINAWEZA” kuwa mtu maarufu! Hii itakusaidia sana kupata moyo na nguvu ya kuendelea kufanya jambo unalolifanya hata kama ni gumu kiasi gani pia wape watu hamasa ya kuendelea mbele. Mkumbuke Barak Obama na Hamasa ya “YES WE CAN”. Pia pale unapokosea jikosoe. Ila nakushauri usijilaumu, bali jiulize kwa nini hili limetokea na nifanye nini ili lisitokee tena. Nakushauri hapa usitumie muda mwingi sana kulaumu na kulalamika. Jifunze kitu kutokana na kosa lililojitokeza- lirekebishe halafu songa mbele kumbuka ‘MAKOSA NI SEHEMU YA MAFANIKIO NA SIYO SEHEMU YA KUSHINDWA’ Nasoma habari ya mtu aliye gundua balbu tunazo tumia kwenye nyumba zetu kutupa mwanga. Wanasema alikosea zaidi ya mara 1000, hata mara ya mwisho alipatia na alipoulizwa: Unasemaje juu ya wewe ulivyoshindwa kutengeneza balbu imara zaidi ya mara 1000? Jibu lake lilikuwa “sijashindwa kutengeneza balbu imara zaidi ya mara 1000, ila nimegundua njia zisizo sahihi zaidi ya 1000 ambazo ukitumia huwezi kufanikiwa kutengeneza balbu imara.” Hamasa inaweza kutolewa kwa njia ya vikao vifupi vilivyo andaliwa kwa lengo maalum la kutoa hamasa. Pia yaweza kutolewa kwa njia ya nyimbo zenye kusisimua na kadhalika. Motisha- (motivation) Wewe kama kiongozi jifunze kutoa motisha. Kuna watu hata ukifanya vizuri kiasi gani hawezi kukusifia! Sana akikusifia anakuambia ah, umejaribu. Kiongozi anatakiwa kuwa mtu anayetambua mchango wa kila mtu katika eneo lake la kazi. Kuanzia wafagia ofisi, makarani, madereva hadi viongozi wa juu. Kila mtu anatakiwa ajione kuwa ni sehemu ya mafanikio au matatizo ya kampuni. Wape watu motisha, mapumziko, barua ya pongezi au chochote kinacho wapa watu motisha. Kama ni wewe mwenyewe nenda kwenye hoteli nzuri wewe na familia pale unapofikia lengo zuri, kama huna uwezo kwa sasa basi jipongeze jinunulie hata soda moja baridi na ujisikie kuwa kweli unajipongeza. Jitahidi sana kutoa motisha iwe ni motisha hasi au chanya. Cha msingi tu ni kuangalia hasa unapo toa motisha hasi usiwe na pupa, fanya uchunguzi, usikurupuke. Wajue watu wako wakati mwingine mtu anaweza kufanya makosa kutokana na mambo yanayo msibu kwenye familia au jamii au hata kwenye eneo lake la kazi. Jitahidi kumsaidia kutatua pale inapowezekana. Asikudanganye mtu kama unataka kutengeneza pesa ya uhakika lazima ujifunze kuwa kiongozi na kuongoza watu. Mara zote viongozi hulipwa zaidi kuliko wafuasi. Usikubali kuwa mfuasi uwe kiongozi. Jifunze zaidi kwa watu ambao ni viongozi, hudhuria mafunzo ya uongozi. Ukifanya hayo utaishia kuwa kiongozi bora. Asanteni sana. Mika Ayo - Mwalimu

Wednesday, March 23, 2016

JINSI YA KUWAPATA WATU WAPYA KWA AJILI YA URAFIKI NA AU BIASHARA



Wapendwa wasomaji wa makala zangu.
 Karibuni sana kwenye darasa letu hili la kujikwamua kimaisha.
Leo nimeamua tuzungumzie suala la jinsi ya kuwapata marafiki, hasa watu wageni au watu ambao tungependa kuwafahamu au watufahamu kutokana na umuhimu wao kwetu na kile tunachokifanya au tunachotarajia kukifanya. Mara nyingi watu hushindwa kuanza au kuanzisha mazungumzo na watu kwa njia sahihi na mwisho huishia kuwapoteza watu ambao wangekuwa muhimu sana kwenye maisha yao.

Hivyo kama ungependa kupata mbinu hizi karibu usome makala hii. Mbinu hizi zitakusaoidia si, tu kupata marafiki lakini pia itakusaidia kupata wateja wapya katika biashara yako.

JINSI YA KUFANYA
1.       Unaweza kukutana na mtu kwenye basi au hospitalini au mahali popote. Kwanza msalimie na ujitambulishe jina lako na kumuomba akuambie jina lake. Akisha jitambulisha nenda hatua ya pili ya mazungumzo yenu.
2.       Mwambie habari ya Familia yako. Mfano mimi nimeoa na nina watoto watatu wawili na mdogo wa mwisho ni wa kiume. Vipi wewe mwenzangu? Ataanza kukueleza kuhusu familia yake na kama hapendelei sana kuhusu kueleza mambo ya familia basi unaweza kukatisha sehemu ya mazungumzo kwa kuendelea sehemu ya tatu ya mazungumzo yenu ambayoni :
3.       Kumjulisha kazi au biashara unayoifanya na kumtaka yeye naye akueleze juu ya kile anachokifanya.  Akisha kukueleza jitahidi sana kusifia kitu kutoka yale aliyo kueleza. Kwa mfano kama amekuambia yeye ni daktari wa binadamu basi mwambie ah! kazi yako ni nzuri sana, naamini kati ya watu wanaofanya wajibu nyeti na muhimu ni madaktari. Au kama ni mfanyabiashara basi sifia kwa vyovyote kile wanachokifanya.
Kwa kufanya hivyo utamsogeza karibu zaidi na wewe kwani ataona kuwa amethaminiwa sana.
Kufikia hapo mtakua mmesha anzisha mahusiano na kama umecheza karata yako vizuri mtakuwa mmeshapeana namba za simu na kupeana miadi ya siku nyingine ya kukutana ili mwendeleze mazungumzo yenu. Pia kama una biashara yako ambayo ungetaka kumshirikisha/ kumuuzia basi mtakuwa mmeshakubaliana jinsi ya kuifanya katika hatua za awali. Kama kufikia hapa bado hujampata kwa maana ya kumshirikisha biashara yako basi nenda kwenye hatua ya nne nay a tano kama ifuatavyo:

4.        Burudani
Kuna baadhi ya watu ambao katika kuongea nao wao hawafurahi sana wakisikia neno BIASHARA kwani wao hujiona kuwa sio wafanyabiashara ingawa kwa namna moja ama nyingine kila mtu ni mfanyabiashara. Ila wao hupenda baadhi ya burdani, kama vile mziki, mpira wa miguu, pool table na kadhalika. Ukiona anahamasika  kwenye hatua hii basi angalia jinsi ambavyo kile unachokifanya (biashara yako) inaweza kumsaidia katika kufanikisha burdani yake ikamfaa zaidi. Kama biashara yako haiingii hapo usilazimishe mambo ishia hapo tu kwa kumpata rafiki kwani huenda siku moja atakufaa katika jambo jingine. Lakini ukiona bado hujampata ili aweze kuwa mteja au kujiunga ili mfanye biashara kwa pamoja nenda hatua ya mwisho ya tano:

5.       Hamasa
Watu tofauti huamasishwa na mambo tofauti tofauti ingawa watu wengi sana huamasishwa na kupata kipato cha ziada kwa maana ya ‘PESA’.  Kama ukishajua kuwa huyu mtu anahamasishwa na nini basi mweleze/ muonyeshe jinsi biashara yako inavyoweza kujibu swali lake/hamasa yake.
Watu wengine huamasishwa na kutoa huduma kwa jamii.
Fuata pia kanuni hizi unapo zungumza na watu:
·         Tabasamu – tabasamu husaidia sana kumuondolea unayezungumza naye hofu au wasiwasi kwani siku hizi kuna matapeli wengi. Ila kama utakuwa na tabasam la bashasha basi husaidia mwenzako kujenga kukuamini na kuwa karibu zaidi na wewe.
·         Usiulize maswali kama ya polisi – acha muda upite kidogo mpe msikilizaji wako muda kidogo wa kutafakari uliomuuliza usiongee kama cherehani pia msikilize na mwache aulize maswali ili ajenge kukuamini. Ingawa unatakiwa kuwa mwangalifu katika sehemu hii ya maswali hakikisha wewe ndiye unaye uliza zaidi katika hatua za awali.
·         Ukiona mtu hataki kukusikiliza usilazimishe, jaribu kuanzisha mazungumzo na mtu aliyeko jirani yenu na yule mtu akikuelewa unaweza kushangaa kupitia jirani yenu yule uliyetaka kuzungumza naye anajileta mwenyewe kutokana na mazungumzo mazuri anayo yasikia kutoka kwa wewe na jirani yenu.
Kumbuka binadamu amafundishwa tangu akiwa mdogo kufanya au kutoa kitu anapo ombwa ndiyo maana ukiulizwa jina utasema jina lako. Ukiulizwa njia ya kuelekea eneo unalolijua na mgeni unatoa msaada nakadhalika.
Ukitaka kujua zaidi juu ya hili soma makala yangu inayozungumzia : JINSI YA KUPATA CHOCHOTE UNACHO TAKA.
Nakutakia kila la kheri katika kukuza idadi ya marafiki kwa kutumia mbinu hizo hapo juu, na nyingine ili uongeze idadi ya marafiki zako na idadi ya wateja wako na idadi ya watu watakaokusaidia kwenye bisashara yako.
Asanteni sana
Mika Ayo.  

Monday, March 21, 2016

JINSI YA KUPATA WAZO LITAKALO KUPATIA PESA



Habari za leo ndugu zangu,
Leo napenda nizungumzie jambo moja muhimu sana katika maisha yetu.
Jambo hilo ni “WAZO”  kwa Kiingereza wanaita ‘Idea’.  Kama nilivyo wahi kusema kila mtu ukimuuliza kwa nini hajafanikiwa kwa kiwango anachotakiwa atakuambia kuwa tatizo ni ‘PESA’  hana kabisa au hazitoshi!
Lakini kwa kweli mara nyingi kama sio mara zote, tatizo huwa siyo ukosefu wa pesa bali huwa ni ukosefu wa “WAZO” sahihi litakalo kupa pesa.
Hivyo leo nataka tuone jinsi ya kupata wazo ambalo litaweza kukupa pesa.
Kabla sijakupa mbinu za kupata wazo ambalo laweza kukupa pesa na siyo pesa tu, bali hata utajiri ngoja nikupitishe mahali fulani ili uweze kufungua macho yako vizuri zaidi kupitia maswali haya:
Je, unajua kuwa dawa ya meno unayotumia ni wazo la mtu? Kuna mtu aliwaza kuwa watu wanahitaji kusafisha vinywa vyao hivyo akapata wazo la kutengeneza dawa ya meno.
Je, unajua kuwa Amerika iligunduliwa na mtu ambaye alikuwa na wazo kuwa kama akisafiri kuelekea magharibi atafika kwenye nchi ambayo hakuna baharia aliyewahi kuifikia? Christopher Columbus alikuwa mtu huyo na kupitia wazo lake hilo alifika Amerika siku moja, nchi mpya. Kwa nini alikuwa na wazo la kufika nchi mpya na pia kutafuta njia fupi ya kuifikia India lakini akafika Amerika na ukawa ugunduzi wa kihistoria kutoka na “wazo”!
Ili uweze kupata wazo zuri litakalo kupatia pesa jifunze kufanya yafuatayo:-
1.       Jifunze kuona kupitia akili yako na siyo macho yako.
 Namaanisha unapokuwa unatembea unaposikia watu wakilalamikia kuhusu hali fulani, au unaweza kuona jambo fulani ambalo haliko sawa basi anza kujiuliza kwa nini hali iko hivyo. Kupitia kujiuliza kwako tayari utashangaa unapata WAZO la kukabiliana na tatizo husika ambapo wengi huita “FURSA”

2.       Andika juu ya wazo lolote zuri linalokujia kwenye ubongo wako
Watu wengi huwa wanapata mawazo mazuri ambayo yangeweza kubadilisha maisha ya mamilioni ya watu wakaishi kwenye hali bora zaidi, lakini kwa kuwa hawajajizoeza kuweka kumbukumbu muda mfupi tu mawazo hayo hupotea.

3.       Soma vitabu
Jambo jingine linaloweza kukusaidia kupata wazo ambalo laweza kukufanya kuwa milionea ni kusoma vitabu. Hapa simaanishi usome vitabu vya tamthilia, HAPANA namaanisha vitabu vya maarifa mbalimbali. Kwa mfano ukitaka kujua Barak Obama rais wa sasa wa Amerika (Barak Obama alikuwa madarakani 2008-2016) nenda kasome vitabu vyake na hasa hii inawafaa wale watu wanaotaka kuwa wanasiasa mahiri.
Ukitaka kujua jinsi Warren Buffet alivyo faulu kuwa tajiri mkubwa huko Amerika soma habari zake. Ninacho jaribu kukuambia hapa ni kwamba kupitia kusoma vitabu vya watu mbalimbali utashangaa unaanza kupata wazo lako la namna ya kutoka kimaisha.

4.       Safiri
Kusafiri ni mbinu nyingine ya kupata wazo la kukutoa kimaisha. Watanzania wengi hatupendi au hatuna kawaida ya kusafiri. Mtu akisafiri ni kwa sababu kuna shida fulani imemsukuma kufanya hivyo!
Jambo hili siyo sahihi kabisa, hebu jizoeze kusafiri kwa lengo la kujifunza na kupitia safari hizi utashangaa utapata wazo la biashara ambalo litakutoa kimaisha.

5.       Anzisha mjadala wenye lengo maalum
Njia nyingine ya kupata wazo ni kuanzisha mjadala kwa lengo la kupata wazo jipya. Mbinu hii unapaswa uitumie kwa watu ambao wamekuzoea kwa mfano wanamichezo wenzako, marafiki zako, wafanyakazi wenzako na kadhalika.
Unaweza kuanza kwa kuuliza maswali yafuatayo (huu ni mfano tu)
Je, miaka mitano au kumi ijayo huu mji wetu utakuwa na tatizo gani kubwa?
Je, ni nini kinaweza kufanyika ili kuweza kukabiliana na hali hiyo wakati huo? (WAZO)
Utashangaa kwa njia hizi nilizo eleza hapo juu unaweza kuja na wazo zuri sana la kukutoa kimaisha.

Kuanzia sasa usikae tu, anza kuchukua hatua.
·         Uwe na tabia ya kutembea na kalamu na karatasi na uandike kila wazo zuri linalokujia na jaribu kufanya utafiti juu ya namna ya kulitekeleza
·         Uwe na tabia ya kujisomea, jifunze juu ya watu waliofanikiwa jinsi walivyo fikia hatua hiyo
·         Nenda kaongee na mtu aliyefanikiwa muulize mbinu alizopitia hadi kufikia mafanikio yake
·         Uwe mvumilivu katika kutekeleza wazo lako kumbuka Roma haikujengwa kwa siku moja
Mwisho niseme tu kuwa njia za kupata wazo zuri ziko nyingi hizo nilizo zitaja ni baadhi tu.
Kumbuka kuwa wenye fedha yakiwepo na mabenki hawatoi pesa kwa ajili ya kuanzisha biashara mpya.
Lakini hutoa pesa kwa ajili ya kutekeleza wazo bora la Biashara mfano mzuri ni wa Ndugu Regnald Mengi. Amekuwa akitoa pesa kwa ajili ya kusaidia vijana wenye mawazo kama hayo. Siyo hilo tu hata
Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakiwezesha mawazo mapya ya ubunifu .
ACHA KUWAZA UTAPATA WAPI PESA WAZA NAPATAJE WAZO ZURI LA KUTATUA TATIZO LA JAMII.
Ukipata wazo zuri zaidi umepata kitu cha thamani sana hata kuliko mgodi wa dhahabu kama unadhani nakutania nenda kawaulize wafuatao:
Wamiliki wa kampuni ya Coca Cola, Mmiliki wa Facebook, Mmiliki wa Microsoft, Mmiliki wa Mohamed Enterprises, Mmiliki wa IPP Media na wengine. Pesa iko kwenye utatuzi wa matatizo ya watu na matatizo ya watu hutatuliwa kwa wazo moja tu la ubunifu.
Kazi ni kwako na kwangu kutafuta “WAZO”
Asanteni. 

Sunday, March 20, 2016

JINSI YA KUTUMIA MUDA/ WAKATI VIZURI

Habari za leo ndugu zangu.
Leo napenda kuzungumzia jambo moja muhimu sana. "JINSI YA KUTUMIA WAKATI"
Watu wengi hatutumii muda wetu vizuri. Mara nyingi utakuta tumebanwa na kazi na inaonekana kana kwamba muda hautoshi.
Yako mambo mengi yanayosababisha sisi kuona kama muda hautoshi na leo nitazungumzia machache sana kati ya mengi.
1. Kupiga stori wakati wa kazi.
Utakuta watu wanapiga stori wakati wa kazi na kujisahau kabisa kuwa huo ni wakati wa kazi na sio wakati wa kupiga stori. Utakuta watu wamekaza mazungumzo kuhusu timu fulani ya hapa nyumbani au ya huko majuu. Yani mtu anajipa cheo cha usemaji wa timu ilhali hata kadi yenyewe ya uanachama wa timu hiyo hana!

2. Jambo la pili ni mitandao ya kijamii.
  Hii mitandao ya kijamii ndio imeharibu watu kabisa, utakuta hata ukizungumza na mtu jambo la maana yani hana hata muda wa kukusikiliza macho yote kwenye smartphone! Jamani ukifuatilia anacho angalia sio hata jambo la maana anaangalia post za kitchen party jambo ambalo angelifanya wakati wa usiku akiwa kapumzika nyumbani (japo kuwa hata hilo sikushauri hasa kama una usongo wa kutoka kimaisha.) Kuna msemo unaosema hivi "SMARTPHONE IS FOR SMART PEOPLE" kuna watu wanazitumia smartphone kupiga hela hao ndo majembe natamani uwe miongoni mwao.

3. Kutokuwa na kipaumbele 
Jambo jingine ambalo linatupotezea muda ni kuto kua na vipaumbele. Unaweza kujikuta unafanya jambo ambalo lingeweza kusubiri wiki ijayo na ukaacha jambo muhimu ambalo lingehitaji kulitatua sasa hivi!
Ni muhimu kujiuliza kila wakati je, hili jambo ninalofanya ndicho kipaumbele kwa sasa? Kama ndiyo endelea kama siyo acha! Fuata kipaumbele ili kwendana na kasi ya wakati. 


JINSI YA KUTUMIA MUDA VIZURI.
SIKU ina saa 24 sasa ni muhimu sana kujipangia muda wote huu wa saa 24 unafanya nini kama unataka kutoka kimaisha a.k.a Kupata PESA
a) Uwe na mpango mkuu wa maisha yako (watu wengi hawana mipango ya maisha yao)
b) Uwe na mpango wa kazi ( Ofisi nyingi zinayo mipango yao, hakikisha mpango wako wa maisha unakuwa sehemu ya mpango wa ofisi unayofanyia kazi kwa wale wenye kuajiriwa) 
c) Kila siku tengeneza orodha ya mambo ya kufanya kwenye siku husika yaani saa 24 (To do list).
Ukijifunza kwa mtindo huo utashangaa hutakuwa miongoni mwa watu wanao sema ah! tuko hapa tunapoteza wakati tu!
Usipoteze wakati UKOMBOE WAKATI:
ASANTENI

Saturday, March 19, 2016

JINSI YA KUPATA CHOCHOTE UTAKACHO “PESA” N.k



Ndugu wasomaji wa blog yangu karibuni tena ili tushirikishane maarifa juu ya jinsi ya kufanikiwa na kupata ‘PESA’ na mafanikio mengine.
Jinsi ya kufanikiwa
1.       Ili uweze kufanikiwa ni lazima ujue unachokitaka.
Mara nyingi watu huangaika katika maisha na ukiwaona utadhani kuwa wamefanikiwa sana, kumbe! Baada ya muda hawana kitu au kama wanacho; hawana raha! Kwa nini? Ni kwa sababu hawajuhi wanachokitaka katika maisha yao.
Ni vigumu sana kupata furaha katika dunia hii kama hatujuhi tunachokitaka. Tatizo kubwa huanzia nyumbani katika familia zetu. Katika familia zetu za Kiafrika ni rahisi sana kumfundisha mtoto adabu na utii kwa wakubwa na wadogo. Na mara nyingi mtoto anatakiwa kusikiliza anachosema mkubwa lakini yeye siyo rahisi kusikilizwa! Jambo hili limeharibu na kuathiri watu wengi wanapokuwa watu wazima kwani hawakupewa ile haki ya msingi ya kuamua ni nini wanachotaka katika maisha yao, hata pale mtoto anapokuwa yuko sahihi. Mara nyingi wazazi wanapandikiza kile wanachotaka ndani ya watoto wao. Watoto wanapo kuwa watu wazima wanajikuta wanaendesha maisha kwa kufuata mzazi anataka nini, ni kama kufukuza upepo Hawajui watokako wala waendako, hawana mwelekeo, hawana furaha, wamekata tamaa! Hawajui wanataka nini katika maisha kutokana na kukosea toka awali kwenye makuzi yao.

Hawajui watokako wala waendako, hawana mwelekeo, hawana furaha, wamekata tamaa! Hawajui wanataka nini katika maisha kutokana na kukosea toka awali kwenye makuzi yao.

 









Ni lazima ujiulize kuwa je, hivi mimi nataka nini katika maisha yangu? Nataka nini kitokee katika maisha yangu leo, wiki hii, mwezi huu, mwaka huu na kadhalika ili niweze baadaye kupata kile ninachokitaka.

Kama hujuhi unachotaka katika maisha yako ni vigumu sana kujua unapo kipata, unaweza ukajenga nyumba usio itaka kwa kuwa tu kila mtu anajenga nyumba na wewe unayo pesa na utajenga na utaishi ndani yake lakini utashangaa huna furaha! Kwa nini ni kwa sababu  sicho ulicho kihitaji. Utaoa, utasoma, utafanya kila kitu lakini hutapata furaha kwa nini; kwa sababu hujuhi unachokitaka.
Njia pekee ya kujua unacho kitaka ambacho kitakupa furaha katika maisha yako ni kutafuta unacho kitaka! 

Njia pekee ya kujua unacho kitaka ambacho kitakupa furaha katika maisha yako ni kutafuta unacho kitaka! 

 




                                                                                                                                                         
Kitabu cha Biblia kinatufundisha jambo hili vizuri “….tafuteni nanyi mtaona” Luka sura 11 mstari 9 (Luka  11:9) hapo juu nimeeleza juu ya wazazi wanavyoweza kutupotosha juu ya yale tunayoyataka(hapa ifahamike kuwa nazungumzia mambo makubwa katika maisha yetu). Wazazi wanayo sehemu muhimu sana katika kuyaandaa makuzi ya watoto wao kulingana na mahitaji ya jamii wanayo ishi. Ila mimi naona kuwa ni kosa kwa mzazi kumwiingilia mtoto katika maisha yake ya baadaye. Mfano mzuri ni kwamba mzazi anaweza kumchagulia mtoto kazi atakayo ifanya katika jamii atakapo kuwa mtu mzima.  Kutokana na malezi na makuzi mtoto naweza akachukua mwelekeo alio ambiwa na mzazi lakini akawa hana furaha kabisa. Pia hofu katika maisha inaweza kutusababisha tukajiingiza kwenye fani ambazo hatuzipendi. Mfano mzuri ni kipindi hiki cha uhaba wa ajira vijana wengi wanajikuta wanaingia kwenye fani ili tu kupata ajira “PESA”  lakini hawapendi kabisa fani husika. Katika hali kama hii ni vigumu sana kufikia malengo kwani tunajikuta tunafanya jambo tusilolipenda. Ni muhimu tufanye jambo tunalolipenda na kupitia jambo hilo ni rahisi sana kufanikiwa.
Sasa kwa wale ambao bado hamjajua mnachokitaka katika maisha yenu basi hii ni fursa kwenu kuchukua hatua kutafuta kile ambacho mnakitaka katika maisha yenu. Kwa kiingereza wanaita “Soul searching” hii ni kama unafanya kazi ya kuihoji nafsi yako juu ya jambo hilo.
Unaweza kujiuliza maswali yafuatayo:
i)                    Je, mimi ni mzuri katika Nyanja zipi? (kuimba, kuchora, nina uwezo  kuhamasisha watu wakafanya nitakalo, nina uwezo wa kuigiza n.k)
ii)                   Je, nikifanya jambo hili Napata furaha?
iii)                 Je, katika jambo hili naweza kuona mafanikio ndani yake miaka mitano kumi ijayo?
iv)                 Ni nani wanaweza kunisaidia (mentors)
Jambo hili siyo rahisi sana ila tu nakuhakikishia linawezekana.
Unalifanya wewe mwenyewe kwa kujihoji, kusoma vitabu, kuwauliza watu wengine na kadhalika.
Kwanza nikupe hongera kama umeweza kusoma makala hii hadi kufikia hatua hii basi wewe uko juu ya watu 90% hapa duniani hivyo nakuhakikishia ukiendelea na tabia hii ya kusoma machapisho kama haya na vitabu vingine na hasa ukayaweka katika vitendo mambo unayojifunza utafanikiwa sana katika maisha yako kipesa na maongezeko mengine mengi.   

2.       Kanuni ya pili ni “KUOMBA” au “KUULIZA
Neno hili kuomba kwenye Biblia ya Kiingereza limeandikwa “ask”  ambapo kwa tafsiri ya kawaida ya Kiswahili ni kuuliza. Lakini kwa kweli ili wewe msomaji wa makala hii uweze kupata ile faida ninayotaka uipate basi nitakuwa natumia maneno haya yote mawili kulingana na haja itakayo jitokeza.
Watu wengi ukiwauliza kwa nini hawajaanzisha biasha ambazo wana ujuzi wa kuzifanya watakuambia ni kwa sababu hawana mtaji.
Watu wengi wanafikiri kuwa  ‘PESA’ ndicho kikwazo kikubwa cha wao kutofanya yale ambayo wanataka kuyafanya kumbe siyo kabisa!

Watu wengi wanafikiri kuwa  ‘PESA’ ndicho kikwazo kikubwa cha wao kutofanya yale ambayo wanataka kuyafanya kumbe siyo kabisa!







Tatizo linaweza kuwa ni wewe kutokuuliza (kufanya utafiti) kile unacho takiwa kukifanya. Hebu nenda kaulize kwa watu waliofanikiwa kwenye jambo unalotaka kulifanya, utashangaa utakavyo weza kupata msaada wa mawazo na hata pesa za kukusaidia kufanya kile unachotaka.
Usishangae nikikuambia kuwa unaweza kupata pesa kwa kuuliza. Unapo uliza Yule unaye muuliza anayasikiliza pia mawazo yako na akiona kuwa unalo wazo lenye tija yuko tayari kuwekeza kwenye wazo lako! Kwa nini anataka kupata “PESA” na kumbuka kuwa mwenye wazo ni wewe hivyo hana jinsi ya kukuacha lazima akushike mkono ili umongoze katika wazo lako mpate pesa. USIOGOPE ULIZA.
Kuomba pia kunaweza kukutoa kwenye lindi la umasikini. Naomba unielewe hapa kuwa simaanishi kukufanya uwe omba omba au Matonya. Ninacho maanisha ni kuwa nakufundisha saikolojia ya watu!
Binadamu tangu akiwa mtoto amefundishwa kutoa anapoombwa au kujibu anapo ulizwa!
Binadamu tangu akiwa mtoto amefundishwa kutoa anapoombwa au kujibu anapo ulizwa! Usiipoteze nafasi hii ya wazi namna hii itumie utaona maisha yako yanaanza kubadilika!
 Acha kuweka pesa, pesa pesa kwenye mawazo yako. Usiwe mtumwa wa pesa wewe jenga mtazamo kwenye  kile unachopenda kufanya na kufanikisha katika maisha yako utashangaa pesa inakuja kirahisi tu.

Kwa mfano, kama unataka kuanzisha biashara katika eneo fulani (wewe furaha yako ni kutoa huduma kwa wateja wako kwa bei nafuu na kukidhi mahitaji ya watu/wateja)  katika mji wako na shida yako ni pesa ya kupanga chumba cha biashara. Hebu kaa na fikiria kidogo fanya utafiti kama kuna eneo au chumba ambacho kipo wazi ambacho unaweza kukitumia kwa biashara yako. Fikiri jinsi ambavyo kwa kufungua biashara yako mwenye nyumba anaweza kunufaika (pamoja na kwamba hutamlipa kodi) muombe ukitumie kwa muda mweleze hali halisi. Kwa kuwa bianadamu amefundishwa tangu utoto kutoa jibu lazima utafanikiwa. Nakuhakikishia hata kama mtu wa kwaza na wa pili atakataa lakini kuna mmoja atakukubalia. Kwa nini hii ni moja ya Kanuni za maisha kama ilivyo kanuni mbalimbali za kisayansi zinavyofanyakazi hii nayo inafanya kazi vilevile.
OMBA/ULIZA
Nenda ukaifanyie kazi mambo uliojifunza hapa una subiri nini ondoka ….. fuata mafanikio> yako.
Asante.