Saturday, March 19, 2016

JINSI YA KUPATA CHOCHOTE UTAKACHO “PESA” N.k



Ndugu wasomaji wa blog yangu karibuni tena ili tushirikishane maarifa juu ya jinsi ya kufanikiwa na kupata ‘PESA’ na mafanikio mengine.
Jinsi ya kufanikiwa
1.       Ili uweze kufanikiwa ni lazima ujue unachokitaka.
Mara nyingi watu huangaika katika maisha na ukiwaona utadhani kuwa wamefanikiwa sana, kumbe! Baada ya muda hawana kitu au kama wanacho; hawana raha! Kwa nini? Ni kwa sababu hawajuhi wanachokitaka katika maisha yao.
Ni vigumu sana kupata furaha katika dunia hii kama hatujuhi tunachokitaka. Tatizo kubwa huanzia nyumbani katika familia zetu. Katika familia zetu za Kiafrika ni rahisi sana kumfundisha mtoto adabu na utii kwa wakubwa na wadogo. Na mara nyingi mtoto anatakiwa kusikiliza anachosema mkubwa lakini yeye siyo rahisi kusikilizwa! Jambo hili limeharibu na kuathiri watu wengi wanapokuwa watu wazima kwani hawakupewa ile haki ya msingi ya kuamua ni nini wanachotaka katika maisha yao, hata pale mtoto anapokuwa yuko sahihi. Mara nyingi wazazi wanapandikiza kile wanachotaka ndani ya watoto wao. Watoto wanapo kuwa watu wazima wanajikuta wanaendesha maisha kwa kufuata mzazi anataka nini, ni kama kufukuza upepo Hawajui watokako wala waendako, hawana mwelekeo, hawana furaha, wamekata tamaa! Hawajui wanataka nini katika maisha kutokana na kukosea toka awali kwenye makuzi yao.

Hawajui watokako wala waendako, hawana mwelekeo, hawana furaha, wamekata tamaa! Hawajui wanataka nini katika maisha kutokana na kukosea toka awali kwenye makuzi yao.

 









Ni lazima ujiulize kuwa je, hivi mimi nataka nini katika maisha yangu? Nataka nini kitokee katika maisha yangu leo, wiki hii, mwezi huu, mwaka huu na kadhalika ili niweze baadaye kupata kile ninachokitaka.

Kama hujuhi unachotaka katika maisha yako ni vigumu sana kujua unapo kipata, unaweza ukajenga nyumba usio itaka kwa kuwa tu kila mtu anajenga nyumba na wewe unayo pesa na utajenga na utaishi ndani yake lakini utashangaa huna furaha! Kwa nini ni kwa sababu  sicho ulicho kihitaji. Utaoa, utasoma, utafanya kila kitu lakini hutapata furaha kwa nini; kwa sababu hujuhi unachokitaka.
Njia pekee ya kujua unacho kitaka ambacho kitakupa furaha katika maisha yako ni kutafuta unacho kitaka! 

Njia pekee ya kujua unacho kitaka ambacho kitakupa furaha katika maisha yako ni kutafuta unacho kitaka! 

 




                                                                                                                                                         
Kitabu cha Biblia kinatufundisha jambo hili vizuri “….tafuteni nanyi mtaona” Luka sura 11 mstari 9 (Luka  11:9) hapo juu nimeeleza juu ya wazazi wanavyoweza kutupotosha juu ya yale tunayoyataka(hapa ifahamike kuwa nazungumzia mambo makubwa katika maisha yetu). Wazazi wanayo sehemu muhimu sana katika kuyaandaa makuzi ya watoto wao kulingana na mahitaji ya jamii wanayo ishi. Ila mimi naona kuwa ni kosa kwa mzazi kumwiingilia mtoto katika maisha yake ya baadaye. Mfano mzuri ni kwamba mzazi anaweza kumchagulia mtoto kazi atakayo ifanya katika jamii atakapo kuwa mtu mzima.  Kutokana na malezi na makuzi mtoto naweza akachukua mwelekeo alio ambiwa na mzazi lakini akawa hana furaha kabisa. Pia hofu katika maisha inaweza kutusababisha tukajiingiza kwenye fani ambazo hatuzipendi. Mfano mzuri ni kipindi hiki cha uhaba wa ajira vijana wengi wanajikuta wanaingia kwenye fani ili tu kupata ajira “PESA”  lakini hawapendi kabisa fani husika. Katika hali kama hii ni vigumu sana kufikia malengo kwani tunajikuta tunafanya jambo tusilolipenda. Ni muhimu tufanye jambo tunalolipenda na kupitia jambo hilo ni rahisi sana kufanikiwa.
Sasa kwa wale ambao bado hamjajua mnachokitaka katika maisha yenu basi hii ni fursa kwenu kuchukua hatua kutafuta kile ambacho mnakitaka katika maisha yenu. Kwa kiingereza wanaita “Soul searching” hii ni kama unafanya kazi ya kuihoji nafsi yako juu ya jambo hilo.
Unaweza kujiuliza maswali yafuatayo:
i)                    Je, mimi ni mzuri katika Nyanja zipi? (kuimba, kuchora, nina uwezo  kuhamasisha watu wakafanya nitakalo, nina uwezo wa kuigiza n.k)
ii)                   Je, nikifanya jambo hili Napata furaha?
iii)                 Je, katika jambo hili naweza kuona mafanikio ndani yake miaka mitano kumi ijayo?
iv)                 Ni nani wanaweza kunisaidia (mentors)
Jambo hili siyo rahisi sana ila tu nakuhakikishia linawezekana.
Unalifanya wewe mwenyewe kwa kujihoji, kusoma vitabu, kuwauliza watu wengine na kadhalika.
Kwanza nikupe hongera kama umeweza kusoma makala hii hadi kufikia hatua hii basi wewe uko juu ya watu 90% hapa duniani hivyo nakuhakikishia ukiendelea na tabia hii ya kusoma machapisho kama haya na vitabu vingine na hasa ukayaweka katika vitendo mambo unayojifunza utafanikiwa sana katika maisha yako kipesa na maongezeko mengine mengi.   

2.       Kanuni ya pili ni “KUOMBA” au “KUULIZA
Neno hili kuomba kwenye Biblia ya Kiingereza limeandikwa “ask”  ambapo kwa tafsiri ya kawaida ya Kiswahili ni kuuliza. Lakini kwa kweli ili wewe msomaji wa makala hii uweze kupata ile faida ninayotaka uipate basi nitakuwa natumia maneno haya yote mawili kulingana na haja itakayo jitokeza.
Watu wengi ukiwauliza kwa nini hawajaanzisha biasha ambazo wana ujuzi wa kuzifanya watakuambia ni kwa sababu hawana mtaji.
Watu wengi wanafikiri kuwa  ‘PESA’ ndicho kikwazo kikubwa cha wao kutofanya yale ambayo wanataka kuyafanya kumbe siyo kabisa!

Watu wengi wanafikiri kuwa  ‘PESA’ ndicho kikwazo kikubwa cha wao kutofanya yale ambayo wanataka kuyafanya kumbe siyo kabisa!







Tatizo linaweza kuwa ni wewe kutokuuliza (kufanya utafiti) kile unacho takiwa kukifanya. Hebu nenda kaulize kwa watu waliofanikiwa kwenye jambo unalotaka kulifanya, utashangaa utakavyo weza kupata msaada wa mawazo na hata pesa za kukusaidia kufanya kile unachotaka.
Usishangae nikikuambia kuwa unaweza kupata pesa kwa kuuliza. Unapo uliza Yule unaye muuliza anayasikiliza pia mawazo yako na akiona kuwa unalo wazo lenye tija yuko tayari kuwekeza kwenye wazo lako! Kwa nini anataka kupata “PESA” na kumbuka kuwa mwenye wazo ni wewe hivyo hana jinsi ya kukuacha lazima akushike mkono ili umongoze katika wazo lako mpate pesa. USIOGOPE ULIZA.
Kuomba pia kunaweza kukutoa kwenye lindi la umasikini. Naomba unielewe hapa kuwa simaanishi kukufanya uwe omba omba au Matonya. Ninacho maanisha ni kuwa nakufundisha saikolojia ya watu!
Binadamu tangu akiwa mtoto amefundishwa kutoa anapoombwa au kujibu anapo ulizwa!
Binadamu tangu akiwa mtoto amefundishwa kutoa anapoombwa au kujibu anapo ulizwa! Usiipoteze nafasi hii ya wazi namna hii itumie utaona maisha yako yanaanza kubadilika!
 Acha kuweka pesa, pesa pesa kwenye mawazo yako. Usiwe mtumwa wa pesa wewe jenga mtazamo kwenye  kile unachopenda kufanya na kufanikisha katika maisha yako utashangaa pesa inakuja kirahisi tu.

Kwa mfano, kama unataka kuanzisha biashara katika eneo fulani (wewe furaha yako ni kutoa huduma kwa wateja wako kwa bei nafuu na kukidhi mahitaji ya watu/wateja)  katika mji wako na shida yako ni pesa ya kupanga chumba cha biashara. Hebu kaa na fikiria kidogo fanya utafiti kama kuna eneo au chumba ambacho kipo wazi ambacho unaweza kukitumia kwa biashara yako. Fikiri jinsi ambavyo kwa kufungua biashara yako mwenye nyumba anaweza kunufaika (pamoja na kwamba hutamlipa kodi) muombe ukitumie kwa muda mweleze hali halisi. Kwa kuwa bianadamu amefundishwa tangu utoto kutoa jibu lazima utafanikiwa. Nakuhakikishia hata kama mtu wa kwaza na wa pili atakataa lakini kuna mmoja atakukubalia. Kwa nini hii ni moja ya Kanuni za maisha kama ilivyo kanuni mbalimbali za kisayansi zinavyofanyakazi hii nayo inafanya kazi vilevile.
OMBA/ULIZA
Nenda ukaifanyie kazi mambo uliojifunza hapa una subiri nini ondoka ….. fuata mafanikio> yako.
Asante.

No comments:

Post a Comment