Friday, March 18, 2016

JINSI YA KUKWAMUA TATIZO LA UKOSEFU WA PESA
Wapendwa wasomaji wa blog hii,
Karibuni kwanza najiona nimepata heshima sana kwa wewe kutembelea ukurasa huu.
Mimi ni Mtanzania ambaye nimekuwa na mawazo ya kushirikisha wenzangu kile nikijuacho ili waweze kupata faida kwenye maisha yao. Kwa ujumla blog hii itajikita sana kwenye masuala ya utafutaji wa pesa, Jinsi mtu unavyoweza kupata pesa bila kuwa na pesa kwa njia halali!
Mimi ninaye andika hapa naitwa Mika Hezekiel Ayo.
Nimefanyakazi Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa zaidi ya miaka 20. Pia nimefanyakazi kwenye NGOs tofauti kwa zaidi ya miaka 7.
Kwenye maeneo nilikofanyakazi nilifanikiwa sana. Niliwahi kupewa cheti cha mfanyakazi bora. Nimewahi kuanzisha vikundi vya wajasiriamali huko Mpwapwa na wakapata mafanikio makubwa sana. Pia huku kwenye NGO nimeweza kusababisha mabadiliko makubwa hasa kwenye sekta ya maji vijijini ambapo wananchi wameweza kuanzisha vyombo vya watumia maji na kwa sasa vinaendelea vizuri.
Kwa sasa nimeamua kujiajiri mwenyewe na nimeamua nifanye juhudi huku kwenye ajira binafsi mpaka nifikie malengo ya juu ya Uhuru wa Pesa.
Kwa sasa bado sijafika huko lakini ninaamini kuwa iko siku ambayo nitafika huko. Waswahili wanasema PENYE NIA PANA NJIA!
Kwanini blog hii itakuwa ikizungumzia masuala ya jinsi ya kujikwamua ki-fedha?
Siku hizi na hata huko nyuma ukiongea na watu wengi ukawauliza kwa nini hawaendelei watakuambia ni kwa sababu hatuna "PESA"  na sababu zinazo oanishwa na sababu hiyo ni kama vile: Sina pesa kwani sina mtaji wa kuanzisha Biashara, sina pesa kwa sababu sina Kazi.
Na mara nyingi lazima watu hawa wanatafuta mtu wa kumlaumu kutokana na hali walionayo>
Mzazi - Baba/mama hakunipeleka shule; kama angelinipeleka shule leo ningepata kazi na singekua na tatizo la pesa.
Serikali - Serikali hajafanya chochote kuhakikisha kuwa vijna wanapata ajira!
Mke/mume - Mume au mke wangu ndiye amekuwa siyo mwangalifu hata akanifikisha kwenye hali hii mbaya niliyonayo.
Mazingira- Najuta kuzaliwa Tanzania kama ningezaliwa Marekani au Ulaya hali ingekuwa tofauti. Kwa ujumla orodha ya visingizio tulivyonavyo ni ndefu sana.
Lakini ya faa tujiulize swali moja la msingi au angalau mawili.
1. Je, hicho kisababishi cha hali nilionayo je, kweli ndiyo sababu hasa kwamba sina pesa?
2. Je, ni kwa jinsi gani mimi mwenyewe nimechangia katika kuwa kwenye hali niliyo nayo ya kukosa pesa?
Mara nyingi maswali kama haya hutupeleka kwenye kutafakari zaidi juu ya nafsi zetu, mazingira yaliyotuzunguka na baadaye tunaweza kuanza kuona fursa zilizopo za jinsi ya kuondokana na hali tulio nayo.
Blog hii itakuwa ni mahali pa kubadilishana mawazo, kupeana mbinu na maarifa, fursa na namna ya kuzifikia na hata kupata msaada wa kutatua kabisa hali ya watu kutokuwa na pesa.

1 comment:

  1. ongeza ukubwa wa maandishi, post ni nzuri sana, endeleza kazi nzuri.

    ReplyDelete