Sunday, March 20, 2016

JINSI YA KUTUMIA MUDA/ WAKATI VIZURI

Habari za leo ndugu zangu.
Leo napenda kuzungumzia jambo moja muhimu sana. "JINSI YA KUTUMIA WAKATI"
Watu wengi hatutumii muda wetu vizuri. Mara nyingi utakuta tumebanwa na kazi na inaonekana kana kwamba muda hautoshi.
Yako mambo mengi yanayosababisha sisi kuona kama muda hautoshi na leo nitazungumzia machache sana kati ya mengi.
1. Kupiga stori wakati wa kazi.
Utakuta watu wanapiga stori wakati wa kazi na kujisahau kabisa kuwa huo ni wakati wa kazi na sio wakati wa kupiga stori. Utakuta watu wamekaza mazungumzo kuhusu timu fulani ya hapa nyumbani au ya huko majuu. Yani mtu anajipa cheo cha usemaji wa timu ilhali hata kadi yenyewe ya uanachama wa timu hiyo hana!

2. Jambo la pili ni mitandao ya kijamii.
  Hii mitandao ya kijamii ndio imeharibu watu kabisa, utakuta hata ukizungumza na mtu jambo la maana yani hana hata muda wa kukusikiliza macho yote kwenye smartphone! Jamani ukifuatilia anacho angalia sio hata jambo la maana anaangalia post za kitchen party jambo ambalo angelifanya wakati wa usiku akiwa kapumzika nyumbani (japo kuwa hata hilo sikushauri hasa kama una usongo wa kutoka kimaisha.) Kuna msemo unaosema hivi "SMARTPHONE IS FOR SMART PEOPLE" kuna watu wanazitumia smartphone kupiga hela hao ndo majembe natamani uwe miongoni mwao.

3. Kutokuwa na kipaumbele 
Jambo jingine ambalo linatupotezea muda ni kuto kua na vipaumbele. Unaweza kujikuta unafanya jambo ambalo lingeweza kusubiri wiki ijayo na ukaacha jambo muhimu ambalo lingehitaji kulitatua sasa hivi!
Ni muhimu kujiuliza kila wakati je, hili jambo ninalofanya ndicho kipaumbele kwa sasa? Kama ndiyo endelea kama siyo acha! Fuata kipaumbele ili kwendana na kasi ya wakati. 


JINSI YA KUTUMIA MUDA VIZURI.
SIKU ina saa 24 sasa ni muhimu sana kujipangia muda wote huu wa saa 24 unafanya nini kama unataka kutoka kimaisha a.k.a Kupata PESA
a) Uwe na mpango mkuu wa maisha yako (watu wengi hawana mipango ya maisha yao)
b) Uwe na mpango wa kazi ( Ofisi nyingi zinayo mipango yao, hakikisha mpango wako wa maisha unakuwa sehemu ya mpango wa ofisi unayofanyia kazi kwa wale wenye kuajiriwa) 
c) Kila siku tengeneza orodha ya mambo ya kufanya kwenye siku husika yaani saa 24 (To do list).
Ukijifunza kwa mtindo huo utashangaa hutakuwa miongoni mwa watu wanao sema ah! tuko hapa tunapoteza wakati tu!
Usipoteze wakati UKOMBOE WAKATI:
ASANTENI

No comments:

Post a Comment