Thursday, May 18, 2017

JINSI YA KUFANYA BIASHARA YA MTANDAO

Habari za leo ndugu zangu.
Leo nataka tuzungumze kwa kifupi juu ya biashara ya MTANDAO. Baadhi ya watu wakisikia biashara ya "mtandao" hufikiri kuwa kinacho zungumzwa ni biashara ya mtandao wa kompyuta! Kumbe! Sio kabisa. Ingawa komputa kupitia intaneti, pia simu kupitia kile kinachoitwa mitandao ya kijamii huweza kuwaunganisha watu na wakafanya mtandao wa namna moja ama nyingine lakini Biashara ya Mtandao ni kitu tofauti kabisa.

Biashara ya Mtandao ni Nini?
Biashara ya mtandao ni mtindo wa kuuza bidhaa au huduma kwa njia ya mtu mmoja kumshirikisha mtu mwingine kwa njia ya mdomo au email au njia yoyote nyingine bila kuwepo kwa mtu wa kati yaani middle man na kama aliye shirikishwa akikubali hujiunga kwenye biashara chini ya ulezi wa yule aliye mwalika. Mara nyingi mwanachama ambaye hujulikana kama msambazaji wa kampuni fulani huwa ndiye: Mteja namba moja wa bidhaa au huduma anazo uza au kusambaza. Pia yeye huwa ndiye Bango la matangazo la kampuni anayoiwakilisha. Hivyo basi huu ni mtandao (muunganiko wa watu) unaofanyakazi pamoja ili kutimiza malengo yao tofauti ingawa wote wako kwenye biashara moja. Kwa kifupi Biashara ya Mtandao ni muunganiko wa watu wanaotumia, kuingiza wanachama wapya na kusambaza bidhaa za kampuni husika.

Ni Nini Watu Wengi Wasichoelewa kwenye Biashara ya Mtandao?
Jambo moja linalo watesa wasambazaji wengi kwenye biashara ya mtandao ni kutumia mtindo wa kibiashara walio uzoea kwenye biashara za kawaida na kuuleta kwenye biashara ya mtandao. Hapa ninamaana kuwa watu wengi huwekeza nguvu kubwa kwenye kuuza zaidi kuliko kusajili.
Tatizo hili linatokana na watu wengi kutokujua hasa ni nini madhumuni ya msingi ya biashara ya mtandao.

Dhumuni kubwa la biashara ya Mtandao ni kuhakikisha kuwa una watu wengi wanokufanyia kazi yaani ningeweza kuwaita wafuasi wako au huitwa down liners kwa kingereza. Kwa kuwa moja ya lengo kubwa la biashara ya mtandao ni kuhakikisha kuwa kila mtu aliyejiunga anatumia kwanza bidhaa/ huduma za kampuni basi kadri unapokuwa na wafuasi wengi basi hata bila kuuza utajikuta kuwa umepata fedha ya kutosha kwenye biashara yako kutokana na manunuzi ya kawaida ya timu yako au wafuasi wako.
NB: Usije ukaichukia biashara hii kwa kuona kama utakuwa unamfanyia mtu kazi la! kazi yoyote unayoifanya ni kwa manufaa yako 100% kwani ukiuza bidhaa unalipwa, ukiingiza mwanacha mpya kwenye biashara unalipwa na baadaye mwisho wa siku kampuni inakupa gawio la faida waliopata. Ni tofauti kabisa na biashara za kawaida ambapo pia hawa watu wenye makampuni ya bidhaa tunazo uza kama vile sukari, soda, nguo nk huwa tunawafanyia kazi na tunachokipata ni lile punguzo la bei ambalo tutalipata kupitia kwa wateja wetu. Basi hakuna kingine!
 
Mfano kama timu yako ina watu 10,000 na watu hawa wakanunua bidhaa za wastani wa shilingi 20,000 kwa mwezi kwa kila mmoja na tuseme kampuni ina sera ya kulipa fidia ya asilimia 5% kwa mauzo ya timu yako hapa utapata TZS 10,000,000 kwa mwezi na pengine wewe umenunua bidhaa za TZS 200,000 kwa mwezi husika!

Hivyo kazi kubwa ni kuandikisha/ kusajili wanachama wapya kuliko kuuza. Kwa nini kuuza kwanza usingeweza kuuza peke yako kiasi hicho kikubwa cha bidhaa kwa mwezi. Pili hata kama unaweza kuuza bidhaa ambazo zinakuwezesha kujikimu kimaisha kwa kipindi fulani, bado una kuwa umekiuka malengo ya biashara ya mtandao. Kwa nini hii inakuweka uwe sawa na mtu mwenye maduka au biashara za kawaida au waajiriwa! Hili siyo lengo, lengo la biashara ya mtandao ina lenga kukuwezesha kuingiza fedha kama unafanya kazi au unaumwa bado fedha zinaingia alimradi tu uwe umesha pata wafuasi au timu kubwa ya kutosha yaani kipato kikubwa kwa kazi kidogo!.

Mbinu zifuatazo zinaweza kukusaidia

a) Onyesha Fursa
Watu wengi hawawezi kunyesha fursa ilioko kwenye biashara ya mtandao. Mtu akigundua kuwa kama akiweka muda wake hapo mwisho wa siku atajikwamua kimaisha basi wangeipokea biashara hiyo na kunufaika na fursa zilizopo

b) Ongea na watu wengi iwezekanavyo
Haitoshi tu kuongea na watu wachache ongea na watu wengi iwezekanavyo.
Jifunze kukataliwa bila kukata tamaa. Watu wengi huchukia au kuogopa kuendelea kuonyesha fursa pale wanapo kataliwa. Siri hapa ni kuendelea ujue kuwa kati ya watu 100 utakaowaambia fursa yako 10 watasikiliza, 5 watataka kujua zaidi na pengine 2 tu ndiyo watakaojiunga! Hivyo jipange na usikate tamaa.

c) Usiache kujifunza.
Kitu kingine watu wengi hufikiri kuwa wanajua kila kitu na hawana haja ya kujifunza. Kumbe wanapotea. Kila siku kunamabadiliko na ili uweze kuendana na mabadiliko unatakiwa kujifunza kila mara.
Nikutakie mafanikio mema kwenye BIASHARA YAKO YA MTANDAO.
Jaribu hii hapa
http://bitcoinslip.com/?hash=36546

Asanteni sana ni mimi
Mwalimu
Mika Ayo

No comments:

Post a Comment