Wednesday, May 3, 2017

Jinsi ya Kupambana na Woga

1. Toka Nje ya Chumba/ Nyumba

Haiwezekani kuwaza vizuri wakati umejawa na hofu na wasiwasi. Jambo la kwanza la kufanya ni kutoka nje na kukaa kwa muda nje ya mazingira yako ya kawaida hadi utakapo tulia kabisa.
Jipe mapumziko ya dakika 15 mbali na jambo linalokupa hofu au woga kwa kutembea kuzunguka jengo la ofisi/nyumba unaweza pia kunywa chai au unaweza hata kwenda kuoga.

2. Vuta Hewa Nyingi

Kama moyo unakuenda mbio au jasho linaanza kutoka kwenye viganja usijaribu kuzuia.
Baki palepale na endelea kujisikilizia bila kushughulikia hali hiyo.
Baada kama dakika moja ama mbili weka kiganja cha mkono wako tumboni na anza kuvuta hewa taratibu, kwa kuvuta hewa ndani kwa wengi kuliko kawaida na kuiachia itoke nje taratibu.
Lengo ni kujaribu kuzisaidia akili zako kuzoea hali ya mashaka iliyojitokeza na kuweza kuchukuliana na hali halisi na baadaye kuondoa hofu.
Kama unaweza tembelea breathing technique for stress.

3. Kabili Unachokiogopa

Kujidai kutojali huweza kufanya hali kuwa mbaya zaidi. Lolote linalo kutatiza na kukuogopesha kama utaamua kulikabili huanza kuonekana jambo la kawaida. Kama kuna siku ulipata woga kutumia lifti au kuvuka daraja refu jaribu kurudia tena na tena hadi utazoea. Fanya hivi kila siku na utaona limekuwa ni jambo lakawaida.

4. Fikiria Jambo Gumu na Baya kukupata

Unaweza kufikiri kuwa unakaribia kupata ugonjwa wa moyo – labda ni kutojiamini tu kuwa utapata ugonjwa wa moyo. Halafu anza kuwaza kuwa wewe huwezi kabisa kwa njia yoyote kupata ugonjwa kama huo. Jitahidi kukabiliana na woga utashangaa woga na hofu vitaondoka.

5. Ikabili Hali Halisi

Huwa wakati mwingine ni vizuri kukabilianan na mawazo ya woga, Kwa mfano unaweza kufikiri kuwa unaweza kukwama kwenye ngazi ya umeme (lift) ya kupanda ghorofani na ukakosa hewa na kufa! Lakini jaribu kujihoji je, uliwahi kusikia mtu aliye pata na mkasa kama huo? Na je kama unaye rafiki mwenye hofu kama hiyo ungemsaidiaje? Jitahidi kuondoa Uoga wa namna yoyote na utashangaa hofu itaondoka na utakuwa huru.

6. Usijaribu Kujifanya Sahihi wakati wote

Maisha yamejaa changamo, ingawa wengi wetu hujihisi kuwa kuwa maisha yao yangekuwa sahihi. Ujue tu kuwa siku mbaya na vikwazo viko siku zote hivyo ni vizuri kujua kuwa maisha ni mchakamchaka.

7. Waza Kama Uko Mahali Pazuri


Hebu kwa dakika moja fumba macho na fikiria kwamba huko mahali pazuri na salama na palipo tulia. Inaweza kuwa unawaza kwamba unatambea ufukweni au uko kitandani na paka (kama wewe ni mpenzi wa wanyama hao) au unaweza kujikumbusha jambo ambalo lilikufurahisha sana wakati wa utoto acha hisia hizo nzuri zikufunike hadi ujisikie mwepesi.

8. Ongea

Ukimwambia mtu wako wa karibu kuhusu hofu yako husaidia sdana kupunguza hofu na woga. Kama huna wa kuongea naye nenda kwa mnasihi hawa wanapatikana hasa kwenye ngazi ya Hospitali za Wilaya au kwenye baadhi ya Mashirika yasiyo ya serikali NGO. Au unaweza kutembelea Idara za Usatawi wa Jamii Ngazi ya Wilaya watakusaidia.

9. Fanya Mambo ya Kawaida

Watu wengi hurudia ulevi au hata madawa ya kulevya kama njia ya kuondoa hofu, lakini jambo hili laweza likakufanya ukachanganyikiwa zaidi. Jaribu kufanya mambo ya kawaida kila siku kama vile kujitahidi kulala vizuri kupata mlo kamili, kufanya mazoezi angalao dakika 30 kwa siku na kupumzika hili linaweza kuondoa msongo wa mawazo.

10. Jipongeze

La mwisho hebu jipongeze. Unapofanikisha jambo lolote katika maisha yako hebu jipongeze kwa kujipa zawadi. Nenda kwenye hoteli nzuri jinunulie chakula unachopenda au fanya jambo lolote linalokupa furaha hii husaidia sana kuondoa kutojiamini na Hofu.

No comments:

Post a Comment