Wednesday, May 17, 2017

JINSI YA KUITAMBUA 'FURSA'

Habari za leo ndugu zangu. Ni siku nyingi hatujaongea kwenye huu ukurasa. Nimekuwa na mambo mengi kiasi kwamba wasomaji wangu mnakosa uhondo wa mazungumzo haya.

'FURSA' NI NINI?
 
Leo nataka kuzungumzia maana ya 'FURSA'
Nadhani kila mtu ukimuuliza maana ya hili neno 'FURSA' atakupa tafsiri yake. Na kwangu mimi kila tafsiri inaweza kuwa sahihi kutokana na kila mtu anavyolielewa neno 'FURSA'

Kwangu mimi fursa ni JINSI MTU ANAVYOWEZA kutazama jambo au kitu na kubuni manufaa yake au ya jamii kubwa kutokana na Jambo au Kitu anachokitazama , alichokiona au alichofikiri.
Ni rahisi sana kusikia watu wakisema katika mji fulani au kijiji fulani hakuna 'FURSA'  ya hili au lile. Hii ni kwa sababu tayari wao wanamtazamo au wanacho walicho tarajia kukiona ambao kwao wao ndio 'FURSA' lakini kwangu mimi hakuna mahali kokote duniani hapa ambapo hapana 'FURSA' Tatizo ni kwamba tu, bado hatujafikiri na kutafuta kwa kina juu ya eneo au hali husika ndiyo maana bado hatujaona 'FURSA' iliyopo mahali au katika hali husika.
Ngoja nikupe mifano hai mitatatu (hii ni mifano ya wazi kabisa)

1.  Uwepo wa Bahari
Hapa Tanzania tunayo bahari ya Hindi. Sasa hebu nikupe jinsi watu tofauti wanavyo itazama Bahari hii kama 'FURSA':

a) Wavuvi

 Kwao ni fursa ya kupata samaki kwa ajili ya kitoweo chao na familia na pia watawauzia watu na kupata fedha kwa ajili ya matumizi mengine.

b) Mabaharia 
Wataiona Bahari kama fursa ya kusafirisha abiria na mizigo kwenda nchi nyingine na wao kujipatia kipato kwa ajili ya kazi hiyo.

c) Wafanya biashara ya utalii
Wataona fukwe za Bahari kama mahali pazuri pa kujenga hoteli na pia kuwapeleka watalii na kujipatia fedha. Orodha inaweza kuwa ndefu lakini naomba niishie hapa kwanza.

2. Uwepo wa miji
Hapa kwetu Tanzania pia kuna miji mingi tu ingawa inatofautiana kwa ukubwa lakini watu mbalimbali wanaweza kuona 'FURSA' mbalimbali kama ifuatavyo:

a) Wasafirishaji wa Abiria na mizigo
Kutokana na kuwepo kwa mkusanyiko mkubwa wa watu wasafirishaji wataona kuna fursa ya kusafirisha ABIRIA na mizigo.

b) Watu wa Elimu
Hawa wataona 'FURSA' ya kufungua shule, vyuo na taasisi mbalimbali za kutoa elimu

c) Watu wa Afya
Hawa wataona 'FURSA' ya kufungua hospitali na maduka ya dawa nakadhalika.

Hivyo kabla ya kulalamika hebu bunga bongo kidogo inawezekana hapo ulipo iko 'FURSA' inayokusubiri uitambue ili uweze kubadilisha maisha yako na ya jamii nzima.

tembelea hapa kwenye mtandao huu na ujiandikishe inaweza kukusaidia.

http://bitcoinslip.com/?hash=36546


KARIBU SANA
Mika Ayo
Mwalimu

1 comment:

  1. Nice somo zuri sana.
    Kwa maoni yangu mimi na kwa tafsiri yangu mimi, fursa ni Taswira ya manufaa au faida binafsi au ya jamii ambayo mtu au watu huiona au kuibuni kwa kutazama au kubuni jambo au kitu fulani.

    ReplyDelete