Karibuni wasomaji wa makala zangu.
Leo naomba niwaambie stori moja nilisoma nikiwa mdogo shule ya msingi.
Habari hii inaeleza habari juu ya mtu mmoja mwenye tamaa ambaye tamaa yake ilimtokea puani!
Ngoja nikupe stori:
Huyu mtu alikuwa ni mtu mbangaizaji, na kazi yake kubwa ilikuwa ni kuchonga mawe kwa ajili ya kuuza kwa wajenzi waliokuwa wakifanyakazi za ujenzi hapo mjini. Kama tujuavyo kazi ya kuchonga mawe ya kujengea ni ngumu kwani ni lazima upasue kwanza mawe halafu ndipo uyachonge yawe kama inavyotakiwa. Kazi hii ilikuwa ngumu sana na alipigwa na jua mchana kutwa!
Alitamani kubadili kazi na akiwa kwenye mawazo hayo alimwona mtu mmoja tajiri akiwa amebebwa kwenye machela na watumwa wake kutoka sehemu moja ya mji kwenda sehemu nyingine ya mji kwani zamani hizo hakukuwa na magari. Yule mpasua mawe akatamani na kujisemea kuwa laiti ningekuwa HUYU tajiri anaye bebwa na watumwa. Mara malaika akamtokea na kumwambia basi tangu sasa utakuwa tajiri na utabebwa na machela. Akaanza kubebwa na watumwa kokote aliko taka kwenda! Akawa na furaha sana! Lakini akagundua kuwa wakati mwingine JUA lina msumbua sana linamuunguza na kumnyima pamoja na watumwa kujitahidi ili asipatwe na jua lakini wapi! Kila siku jua linamtesa! Akasema akh! Laiti ningekuwa JUA niwaunguze wanadamu kama linavyoniunguza mimi. Kumbe ! Malaika akamwambia basi WEWE UTAKUA JUA KUANZIA LEO! Basi yule mtu akawa jua. Akawaunguza wanadamu watu wakakosa raha kwa ukali wa Jua wakashindwa kufanya kazi na yule mtu - JUA akafurahi sana lakini siku moja ghafla majira yakabadilika likaja wingu likafunika JUA na mvua ikaanza kunyesha. Jua akahuzunika sana kwani kwa takriban miezi kama mitatu hakuweza kutimiza azma yake ya kuwaunguza akachukia sana na akasema laiti ningekuwa WINGU ili nizuie Jua kuwaunguza watu na kunyesha mvua na kuleta mafuriko na kwa mafuriko nitakayo sababisha basi kila kitu kitasombwa na kutupwa baharini. Kumbe! Mara malaika akamwambia umekuwa WINGU kuanzia leo! Yule mtu alipogeuka wingu akaanza kunyesha mvua na kukawa na mafuriko makubwa sana naye akafurahi sana kuwa kila kitu husombwa na maji ya mafuriko. Lakini baada ya muda akagundua kuwa kulikuwa na mwamba chini ya mlima ambao kila akinyesha mvua huo mwamba hautikisiki. Akajaribu siku nyingi lakini wapi. Hakuweza kuutikisa ule mwamba! Mwisho kama kawaida yake akajiombea awe Mwamba naye akapewa kuwa Mwamba basi akafurahi sana! Mvua ikanyesha hakutikisika, Jua likawaka nalo pia halikufua dafu juu yake akafurahi siku nyingi. Lakini siku moja akaja Mchonga mawe mmoja na mara akaanza kubomoa sehemu ya mwamba Ule, na kuchukua vipande vya mawe na kokoto kwa ajili ya kazi ya ujenzi . Ndipo akakata tamaa na kutamani laiti angekuwa yule binadamu ANAYE PASUA mawe. Kumbe akageuka akarudia hali yake ya kwanza. Ndipo alipo anza kujuta kuwa kumbe amepata nafasi nyingi sana na akuweza kuzitumia.
Kwenye stori hii tunajifunza mambo kadhaa.
1. Kila nafasi katika maisha ya mwanadamu ina faida yake ni wewe tu kujiongeza na kujua nafasi ulioko na kuitumia kikamilifu.
2. Tujua kuwa katika maisha kuna kupanda daraja tatizo siyo kupanda daraja tatizo ni kwamba huwa tunafikiri kuwa eti tukipanda daraja fulani la juu basi changamoto zitakwisha kumbe kila daraja lina changamoto zake kubwa kulingana na hatua au kiwango tulichopanda. Hivyo ni vema tukajua kuwa kupanda daraja ni ngazi ya kupambana na matatizo na changamoto kubwa zaidi. Ni kweli utakuwa na raha za viwango vikubwa zaidi lakini ujue na changamoto zake ni kubwa zaidi!
3. Tujifunze kuridhika na hatua tuliofikia,. tusiwe watu wa kulalamika. Kwani kulalamika kutasababisha kukata tamaa na kurudi viwango vya chini au hata kuwa na hali mbaya zaidi kuliko mwanzo.
4. Tujifunze kwa waliofanikiwa na siyo kutamani kuwa kama wao kwani sisi siyo wao! Kuna mtu mmoja alinishangaza kwenye Ukurasa wa Facebook alimwambia mhamasishaji mmoja nataka kuwa kama wewe! Mwezeshaji akamwambia hapana sitaki uwe kama mimi ila nitakufundisha ili ufanikiwe.
Ni matumaini yangu kuwa Kisa hiki kitakusisimua na kuamsha ari mpya ndani yako ambayo itakuletea mafanikio.
MIKa Ayo - Mwalimu
Sunday, July 3, 2016
Wednesday, June 22, 2016
Kazi au Malipo?
Habari za leo wasomaji wa makala zangu.
Leo naomba ujiulize je? Unacho kifanya ni kazi kwa ajili ya kutimiza hitaji fulani katika jamii au ni kazi kwa ajili ya kujipatia malipo au kipato?
Mimi sijuhi ila jibu unalo wewe lakini ngoja nikuambie faida na hasara za kufanya kazi kwa ajili ya malipo na kufanyakazi ili kujibu hitaji fulani ndani ya jamii.
Faida za kufanya kazi kwa ajili ya malipo
1. Utapata fedha kwa ajili ya mahitaji yako na watoto wako
2. Utalipwa unacho stahili
3. Utapata furaha ya muda mfupi sana
4. Utapata kazi
Hasara zake
1. Hutaridhika na kile unacholipwa kwani wewe unachotaka ni fedha na siyo kutoa huduma!
2. Utajenga maadui ndani na nje ya ofisi kwani wewe unachojali ni Pesa na siyo mahusiano na watu
3. Ukimaliza kazi utasahalika hutakumbukwa tena
4. Utakuwa mtu wa kujilaumu kila wakati
Faida ya Kufanya Kazi kama kazi
1. Utakuwa unajibu hitaji la jamii
2. Utapata heshima kubwa na hutaweza kusahauliwa milele!
3. Utakuwa mwenye furaha maisha yako yote!
4. Utatimiza malengo yako siku zote
5. Utakuwa na marafiki ndani na nje ya ofisi yako.
Hasra za kufanya kazi kama kazi
1. Kutoa muda wako mwingi kwa ajili ya wengine
2. Wale unaofanya kazi nao kukutegea kwani wanajua wewe hutakubali jahazi lizame
3. Unaweza kupoteza haki zako kutokana na kwamba wewe unachojali ni kutimiza wajibu wako na siyo malipo malipo kwako si kitu muhimu. La muhimu kwako ni kutimiza kazi yako.
Hivyo nakushauri uchukue hatua ufanye kazi kama kazi kwani hata kama watakudhulumu haki yako itapatikana au niseme utaipata tu!
Wewe wekeza kwenye jamii siku moja utalipwa hadi ushangae.
Mika Ayo - Mwalimu

Friday, June 17, 2016
Jinsi ya Kuepuka Mateso ya Baadaye
Habari za leo wasomaji wa makala zangu
Kwanza nawashukuru sana kwa kusoma kile ambacho nakiandika humu. Leo naomba niwape siri kwa nini nimeamua kumiliki blogu yangu mwenyewe!
NI ILI NIPATE UHURU WA KIFEDHA
Mimi
niko tayari kuteseka kwa ajili ya kupata UHURU kamili. Robert Kyosaki
mwandishi mashuhuri sana na tajiri na rafiki mkubwa wa Mgombea urais wa
Marekani Donald Trump aliwahi kusema. Freedom is not real freedom
without financial freedom! Rich Dad Poor Dad by Robert Kyosaki
Mimi nimeianza safari hii nikiwa na Miaka zaidi ya 50!
Hii
ni kutokana na kuchelewa kupata taarifa sahihi mapema au basi kwa kuwa
mimi ni muumini mzuri wa dini yangu ya Kikristo nisema huu ndiyo mpango
wa Mungu kwangu.
Ni
meamua kuteseka kwa kuacha kazi serikalini hivyo sina kiinua mgongo
(tangu mwanzo nilichukia na hata sasa nachukia dhana ya kiinua mgongo na
pensheni! Kimsingi sikubaliani na kulipwa mamilioni baada ya mateso ya
maisha yote, umenyanyaswa na bosi mchana kutwa jioni mwenyenyumba unaye, watoto wamefukuzwa shule ada hujalipa n.k eti baada ya mateso yote hayo unapewa shilingi milioni 60 ukiwa na miaka 60! Ili uifanyie nini? ujenge nyumba au ununue matatizo? Maana hukuwahi kushika kiasi kikubwa cha hela maisha yako yote. Ninaamini hutaweza kuimiliki na ndiyo maana wastaafu wengi wanafilisika chini ya miaka miwili hawana kitu!)
Najua stori za akina Colonel Harland David Sanders Wa Kentucky Fried chicken alianza safari hii akiwa na zaidi ya miaka 60 na alifika.
Wako walioanza na miaka zaidi ya 70 wakafika hivyo sina shaka mimi pia nitafika.
Najua kwa msaada wa watu waliofanikiwa sina shaka nitafika cha msingi ni mimi kutokata tamaa.
Pia hata wewe nakushauri usikate tamaa. Njoo tushauriane nini cha kufanya. Usiache kazi kama umeahiriwa wewe fanya lakini uwe na malengo ya maisha hakikisha fedha yako inakufanyia kazi kwa bidii. Kama hujui jinsi ya kuifanya fedha ikufanyie kazi ili ikuzalishie fedha nyingi zaidi uliza kwa watu utapata ushauri wa nini cha kufanya.
Nashukuru sana kocha. Ubarikiwe
Mika Ayo
Saturday, June 11, 2016
UMUHIMU WA KUFANYA UTAFITI
Habari za leo wasomaji wa makala zangu.
Leo nataka nizungumze kwa kifupi juu ya utafiti na umuhimu wake kabla hujawekeza.
Utafiti utakusaidia kujua mambo kadhaa katika biashara au shughuli unayo taka kuwekeza.
Watu wengi huanzisha biashara kabla ya kujua ugumu na changamoto zilizoko kwenye biashara husika!
Watu hujiiingiza kwenye biashara eti kwa kuwa tu ndugu au rafiki yao fulani amefanikiwa kwenye biashara hiyo.
Ngoja nikupe siri moja. HAKUNA MTU ATAKAYE KUONA UKIWA CHINI NAMAANISHA KABLA YA KUFANIKIWA. Mara zote watu watakuona pale unapofanikiwa na huwa hawakumbuki umeteseka miaka mingapi au ni magumu mangapi umepitia kabla ya kufikia hapo ulipo. Wao hufikiri ni rahis kufanikiwa hivyo hukurupuka na baadaye wanapata hasara.
Ili usipate hasara ya muda na fedha na mwisho kukata tamaa na maisha ni vizuri ukafanya utafiti wa kutosha juu ya biashara yako mpya unayotaka kuanzisha.
Utafiti utakusaidia mambo yafuatayo ( haya ni machache kati ya mengi)
i) Kujua ukubwa au udogo wa soko la bidhaa zako
ii) Kujua washindani wako katika biashara na nguvu walionayo kwenye biashara husika
iii) Kujua watu wa kukusaidia ili uweze kuanza biashara husika
iv) Kuamua mchepuo (niche) wa biashara yako kwa mfano kama unataka kuanzisha biashara ya huduma ya kuhudumia watalii basi unaweza kuangalie wewe ujikite kwenye mchepuo gani kutokana na vigezo ulivyo navyo wewe
v) Kujua masuala ya kisheria yahusuyo biashara husika
vii) Kujua hitaji ambalo bado halijatoshelezwa kwenye biashara husika (hii inaweza kuwa ndiyo nguvu na nguzo muhimu sana kwako ambayo itakupa mafanikio kwani utakuwa unawasaidia watu kutatua matatizo au tatizo ambalo bado halijatatuliwa na ukiweza kutoa ufumbuzi basi umepiga BINGO)
viii) Kujua pa kuanzia na mengine mengi
Hivyo nakushauri ndugu yangu usikurupuke kuanza biashara wewe fanya utafiti kwanza ndipo uchukue maamuzi kutokana na taarifa ulizo kusanya kwenye utafiti wako.
Asanteni

Wednesday, June 8, 2016
SIKU ZAENDA MBIO
Japo mwaka wa kesha lakini siku zaenda,
Utadhani bado tupo na muda kumbe siku zaenda,
Huwezi kujua wewe ila siku zaenda
Utakapo lipwa mshahara au siku ya jambo hufika!
Hapo ndipo utatambua kumbe siku zaenda!
Juzi ilikuwa ndo jana na kesho ndo leo!
Kwanini kupoteza wakati na kumbe siku zaenda.
Jitume wa kwetu jitume kwani siku zaenda.
Juzi nilikuwa mtoto na jana nilikuwa baba eti leo mimi BABU!
Ni kwambiayo ni kweli kwani siku zaenda mbio sana!
Jitahidi kutimiza malengo kwani siku zaenda.
Huwezi kuja fidia siku ikishaenda imeenda!
Mika Ayo - Mwalimu ( 0763506835)

Monday, May 30, 2016
JINSI YA KUWAPATA WATU WENGI
Habari za leo ndugu wasomaji wa makala zangu.
Leo nataka kujadili kwa kifupi jinsi ya kuwapata watu wengi zaidi katika biashara yako au kanisa lako au kazi yako.
Kabla sijazungumzia mbinu hizi ni muhimu kujua kuwa mafanikio yetu yanatokana na idadi ya watu tulionao.
Hakuna kazi au shuguli au biashara inayoweza kufanikiwa ikiwa haina watu wa kutosha wanaoiunga mkono!
Ili kuwapta watu tufanye nini?
1. Tuwapende watu
Upendo ni kitu hadimu sana katika maisha ya dunia ya leo. Mara nyingi watu wamekua wakiwatafuta watu wajiunge kwenye biashara zao ili wawafaidi na sio ili wale watu wapate faida itokanayo na bidhaa au huduma wanayo toa. Kama tunawatafuta watu ili tuwafaidi hapa kunakuwa hakuna upendo. Pia tujue kuwa badala ya kujijengea marafiki tunaongeza maadui jambo ambalo halitakiwi kabisa.
Kama tunawapenda watu tutawaonyesha jinsi ambavyo, huduma au bidhaa zetu zinavyoweza kuwabadilisha maisha yao yakawa bora zaidi (ni muhimu kuhakikisha kuwa tunacho waambia ndivyo kilivyo). Kwa kufanya hivyo watu wengi watakuja upande wetu na kutupa kile tunacho taka kwani sisi pia tumewapa wanacho taka. Hii ni kanuni ya maisha.
2. Kufanya ufuatiliaji
Mara chache sana huwa tunafanya ufuatiliaji wa matokeo ya huduma au bidhaa tulio uza ilivyo msaidia au kutomsaidia mteja. Jambo hili ni baya sana kwani kama kuna mteja ambaye alipewa maelezo yasiyo sahihi juu ya namna ya kutumia huduma au bidhaa yetu akaitumia ndivyo sivyo basi mtu huyo atakuwa balozi mbaya kwa upande wa biashara yetu. Lakini kama tunafanya ufuatiliaji itakuwa rahisi kugundua na kufanya marekebisho. Unaweza kutumia njia mbali mbali za kufanya ufuatiliaji ikiwemo kuweka sunduku la maoni, kuandaa hojaji fupi la kuwauliza wateja wako wa mara kwa mara ili kujua wanavyo ridhika au kutoridhika na huduma unayo toa. Kitendo cha kufanya ufuatiliaji huwafanya watu waone kuwa wanajaliwa, wanathaminiwa na wanapendwa hata kama kulikuwa na kasoro iliyojitokeza basi watu huwa tayari kuisahau na kuendelea mbele.
3. Kutoa Motisha
Binadamu alivyo umbwa anapenda sana kupongezwa. Wala mtu yeyote asikudanganye eti kuwa yeye hapendi kupongezwa. Kila mtu anapenda kupongezwa. Ni vizuri kuwapongeza watu walio kuja kutaka huduma kwako. Pongezi ya mdomo tu wakati mwingine inatosha. mfano; karibu tena, asante kwa kututembelea (wapongeze hata kama hawajanunua kitu).
4. Uvumilivu
Ni muhimu sana kuwavumilia watu hata kama wakati mwingine wamekukosea. Usitake kugombana nao tafuta njia muafaka ya kuachana nao kwa amani. Kwani hujui kama mtu huyu ambaye unakuwa adui naye huenda kesho akawa mahali ambapo unahitaji msaada kutoka kwake.
Ndugu Msomaji kwa leo niishie hapa. Nakutakia mafanikio mema kwenye maisha yako.

Wednesday, May 25, 2016
MUDA KITU CHA AJABU SANA
Muda ni kitu cha ajabu sana
1. Kikipotea huwa huwezi kupata tena !
2. Ndiyo nguvu inayoweza kutupa majibu ya matatizo yetu wote na yote!
3. Ndiyo kitu kinachotunzwa kuliko vyote!
4. Ndiyo kitu kinacho haribiwa na kupotezwa kuliko vyote!
5. Ndicho kitu kinacho tumika kuliko vyote hakuna muda wowote mtu yeyote ataacha kutumia muda kufanya chochote!
6. Ndicho kitu kifupi kuliko vyote !
7. Ndicho kitu kirefu kuliko vyote!
8. Ni adui wakati fulani na rafiki wakati fulani!
9. Huwezi kuupunguza muda wa siku ni saa 24 siku zote!
10. Kikienda hakirudi.
TAFAKARI
MIKA AYO - Mwalimu

Subscribe to:
Posts (Atom)