Wapenzi wasomaji wa
makala zangu; habari za leo.
Leo napenda tuzungumze juu ya jinsi ya kujiongeza katika
maisha.
Jambo la kwanza kabisa lazima tujue kuwa kila dakika ya
maisha yetu inayopita kunamabadiliko yanayotokea kwako, kwa kazi yako au
biashara yako. Japo siyo rahisi kuyaona kwa kuwa bado ni mapema kuyaona au
kuyatambua, ingawa utakuja kuyaona baadaye! Kuna mwanafalsafa mmoja wa India
alisema hivi “unapoanza kuvuka mto kila hatua unayopiga kuvuka mto, ule mto
unabadilika na wewe mwenyewe unayevuka unabadilika” .
Alisema kumaanisha kuwa kila sekunde ni sekunde ya
mabadiliko. Hivyo tunachotakiwa kukifanya ni kujiongeza ili tuweze kuendana na
mabadiliko. Tukichukulia mfano wa mto kubadilika kama ungekaa pale pale ndani
yam to kwa muda mrefu kuna siku ungekumbwa na mafuriko. Ndivyo ilivyo katika
maisha yetu kama tusipojiongeza tutajikuta tunaathirika na mabadiliko kwa
kutojiongeza.
Tunajiongeza kwa kusoma mambo mapya kila siku kuhusu kile
tunachokifanya.
Tunajiongeza kwa kuwa wabunifu kuhusu yale tunayoyafanya
tujaribu kubuni njia mpya na bora zaidi ya kufanya lile tulifanyalo ili liwe na
ufanisi zaidi.
Tunajiongeza kwa kuhakikisha kuwa hatuwanufaishi watu
wengine wakati sisi tunazidi kudidimia. Tunawanufaisha waajiri wetu na wanakuwa
matajiri wakati sisi tunabaki masikini (simaanishi usitimize wajibu wako kwa
mwaajiri na maanisha kuwa hakikisha kuwa na wewe unajinufaisha kwa kuweka
mpango wako wa maisha ili usonge mbele).
Tunawanufaisha wauzaji wa bidhaa mbalimbali kwa sisi kuwa wateja na
kuridhika na maisha namna hiyo, badala ya sisi nasi kujiongeza na kunufaika kwa
kuuza bidhaa zetu ili tubadili maisha yetu.
Kwa mfano wengi wetu tuna simu za mkononi na katika simu
hizo tuna watu 250 au zaidi hebu jiulize kati ya hao ni wangapi ni wateja wako?
Namaanisha unaofanya nao biashara na kuingiza kipato. Kwa wale ambao angalau
watu 10 au zaidi kati ya majina yote yaliyoko kwenye simu yako ni wateja wako
nawapa hongera.
Kwa wale ambao bado nawataka mjiongeze, hebu fikiri ni jinsi
gani utatumia watu hao kukuingizia kipato badala ya ku- “chat” tu
bila faida yoyote. Fanya kujiongeza kwenye mitandao ya kijamii ambayo wewe
unaitumia ili unufaike. Kumbuka hizi zote ni fursa za kupata ushauri juu ya
yale tunayoyafanya na pia kupata wateja na kadhalika.
TUJITAHIDI KUJIONGEZA KILA SIKU KWANI KUJIONGEZA KUNAFAIDA
KUBWA SANA.
Asanteni.
Mika Ayo – Mwalimu (+255-763506835 au +255-673506836 email
mikahezekiel@hotmail.com)
No comments:
Post a Comment